30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

IRAN KULIPIZA KISASI MAREKANI IKIFUFUA VIKWAZO

ayatollah-ali-khamenei_1TEHRAN, IRAN

KIONGOZI wa Kiroho wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema Iran itajibu mapigo iwapo Marekani itafufua vikwazo mwezi ujao.

“Katika suala la makubaliano ya nyuklia, utawala wa sasa wa Marekani umefanya ukiukaji kadhaa, karibuni zaidi ikiwa ni ufufuaji wa vikwazo vya miaka10,” alisema Khamenei wakati akiwahutubia maelfu ya wanamgambo wa kujitolea wa Kiislamu wa Basij.

“Iwapo vikwazo vitaendelezwa, itakuwa ni ukiukaji wa JCPOA,” aliongeza akimaanisha makubaliano ya mwaka jana ya mataifa makubwa, ambayo pamoja na mambo mengine yalikubali kufuta vikwazo ili Iran idhibiti programu yake ya nyuklia.

“Wanatakiwa kufahamu kwamba Jamhuri ya Kiislamu itajibu mapigo.”

Wiki iliyopita Bunge la Marekani lilipiga kura kufufua vikwazo vya muda mrefu vinavyohusu jaribio la Iran la kurusha makombora pamoja na rekodi mbaya ya haki za binadamu.

Vikwazo vya miaka 10 bado vinahitaji kupitishwa na Seneta na Rais Barack Obama ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Washington inasema vikwazo hivi havihusiani na makubaliano ya nyuklia, lakini Iran inasema kuviendeleza ni kuua ari ya makubaliano, hasa kwa vile vinazuia kurudi kwa benki za kimataifa.

“JCPOA haipaswi kuwa kifaa cha kukandamiza watu wa Iran,” alionya Khamenei.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles