30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

IPTL YAAMRIWA KUILIPA STANDARD CHARTERED DOLA MILIONI 168.8

Kulwa Mzee-Dar es Salaam

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeiamuru Kampuni ya Kufua Umeme IPTL kuilipa Benki ya Standard Chartered Hong Kong na Benki ya Standard Chartered Malaysia Dola za Marekani 168,800,063.87.

Uamuzi huo   ulitolewa na mahakama hiyo baada ya kukubali kuisajili hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ikiitaka kampuni hiyo kulipa fedha hizo.

Jaji Baker Sehel alitoa uamuzi huo baada ya kuisajili hukumu hiyo hivi karibuni na kuamuru IPTL kulipa fedha hizo.

Alisema  walalamikiwa wanaweza kuwasilisha maombi ndani ya siku 21 ya kutaka usajili huo uwekwe pambeni na taarifa ya kusajili hukumu iwasilishwe kwa walamikiwa ikionyesha haitatekelezwa mpaka zipite siku 21.

Novemba 16 mwaka jana, Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ilisikiliza kesi  hiyo baada ya walalamikiwa kushindwa kuwasilisha utetezi wao.

Walalamikaji katika kesi hiyo walikuwa Standard Chartered Bank Hong Kong Limited na Standard Chartered Bank Malaysia wakati walalamikiwa ni IPTL, VIP Engeneering and Marketing Limited na Pan Africa Power Limited.

Katika shauri hilo walalamikiwa walishindwa kuwasilisha utetezi kwa madai kwamba mtambo wa IPTL na yote yanayohusu kampuni hiyo yako Tanzania na kwamba kabla ya kesi hiyo kuna kesi nyingine mbili nchini.

Inadaiwa msingi wa kesi hizo ni kuhusu uhalali wa Standard Chartered Bank kuwa mdai halalali wa IPTL.

Katika kesi   moja, IPTL na PAP wanaidai Standard Chartered Bank Sh trilioni sita na ya pili, VIP wanaidai benki hiyo Sh trilioni moja.

Pamoja na kuwasilisha pingamizi, mahakama ilitupilia mbali na kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles