24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

INDIA: UCHAGUZI WA BUNGE WAANZA

Wapiga kura milioni 900 wa India waako vituoni kulichagua bunge jipya-zoezi litakaloendelea hadi May 19 inayokuja.

Wapiga kura kutoka majimbo 20 ndio wa mwnazo kupiga kura kati ya awamu saba za utaratibu huo wa uchaguzi. Maelfu ya vyama vinagombea viti katika uchaguzi huo.

Waziri Mkuu Narendra Modi wa chama cha Bharatiya Janata Party-BJP anapewa nafasi nzuri ya kushinda na kuendelea na mhula wa pili madarakani. Anakabiliwa hata hivyo na ushindani mkubwa kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha Congress Rahul Ghandi .

Maoni ya wengi yanaashiria mashindano makali. Vyama vingi vinavyopigania viti katika uchaguzi vinaweza kushawishi muundo wa serikali ya muungano. Hatua za usalama zimeimarishwa kote nchini India.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles