25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ILO yataka taka za kielektroniki zisimamiwe vyema

Shirika la kazi duniani, ILO limetaka hatua za haraka zichukuliwe ili kusimamia vyema taka za kielektroniki zinazozalishwa kote ulimwenguni ili hatimaye ziwe chanzo cha ajira zenye utu.

Wito huo umetolewa katika mkutano wa ILO unaofanyika huko Geneva, Uswisi ambako wawakilishi wa serikali, wafanyakazi na waajiri wamesema wakati umefika kwa serikali kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya kuchakata na kutumia upya taka za kielektroniki kwa kuzingatia kasi kubwa ya ongezeko la taka hizo ambazo kila mwaka huzalishwa tani milioni 50 zikiwa na thamani ya dola bilioni 62.

ILO inasema ni asilimia 20 ya tani hizo za kielektroniki ndio huwekwa katika mazingira rasmi.

Kama hiyo haitoshi, mazingira ambayo wafanyakazi wanaookota taka hizo ili ziweze kuhifadhiwa ni magumu, wakiwa hawana mamlaka yoyote juu ya ujira wa fedha zitokanazo na kazi hiyo ngumu huku wakivunja taka hizo kwa mikono mitupu bila vifaa vya kujikinga.

Nikhil Seth ni mwenyekiti wa jopo la kimataifa la mashauriano kuhusu kazi zenye utu na taka ngumu anasema taka za kielektroniki zinazidi kuwa rasilimali muhimu kwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kwenye mnyororo wa thamani kuanzia kwa wanaoziokota, wanaozitengeneza upya, wanaozitumia tena na wanaleta huduma bunifu na bidhaa kwenye soko na kurahisisha mzunguko wa uchumi.

Seth amesema lazima kuwa na mfumo bora zaidi wa kusimamia taka hizo kuliko hivi sasa ili kuhakikisha kuwa taka za kielektroniki zinazozalishwa kwanza kabisa hazileti aina ya madhara ambayo taka za kielektroniki ambazo hazijachakatwa zinaweza kuleta kwa mazingira, kwa afya ya binadamu na kwa wale wote wanaofanya kazi kwenye viwanda  ya usimamizi wa taka za kielektroniki.

ILO imekumbusha pia umuhimu wa kutumia vijana ikisema kuwa vijana wana  ubunifu mkubwa wa kutumia taka za kielektroniki na hivyo ni fursa ya kuongeza nafasi za ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles