26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

IGP AWAOMBA RADHI WAANDISHI WA HABARI

 

 

Na ABRAHAM GWANDU, ARUSHA

MKUU wa Jeshi la Polisi  (IGP), Ernest Mangu, amesema vitendo vya  polisi kuwakamata waandishi wa habari wanapokuwa katika majukumu yao ya taaluma siyo msimamo wa jeshi hilo bali ni la bahati mbaya.

Alisema waandishi na vyombo vya habari ni wadau muhimu wa jeshi hilo lazima washirikiane nao.

IGP Mangu alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari  baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (Sarpcco) unaoendelea   Arusha.

“Askari anapokuwa katika eneo la tukio anakuwa na tabia fulani ambayo kila mmoja wetu anayo kulazimisha mambo, ninyi ni wadau wetu lazima tufanye kazi pamoja hatuna ugomvi wowote na waandishi.

“Yanapotokea matukio ya aina hiyo ya kukamatwa au kusumbuliwa tujulishane kwa sababu askari wadogo wakati mwingine hufanya vitu ambavyo siyo msimamo wetu sisi viongozi wao,” alisema IGP Mangu.

Mangu pia alizungumzia matukio ya mauaji yanayoendelea wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani akisema ni uhalifu kama ulivyo mwingine wa kawaida na usitafsiriwe vinginevyo kwa sababu   tayari umeanza kudhibitiwa.

Wakati IGP Mangu akisema hivyo, vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 60 katika mahabusu ya gereza la Kisongo kwa tuhuma za kuhusika na ugaidi ikiwamo kurusha bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Massauni alisema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Sadc   kuhakikisha uhalifu wa kuvuka mipaka unadhibitiwa.

Naye Katibu Mtendaji wa Sadc, Stegomena Tax, aliwahakikishia wakuu hao wa polisi  kuwa Jumuiya anayoingoza itaendelea kutoa misaada na ushirikiano kila unapohitajika   kuimarisha usalama katika eneo hilo.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles