24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya watalii kutoka China kuongezeka nchini

Asha Bani

Idadi ya watalii kutoka nchini China inatarajiwa kuongezeka zaidi nchini  mara tu kutakapoanza kwa safari za ndege kutoka Dar es Salaam hadi nchini humo jambo linalosubiriwa kwa hamu na taifa hilo.

Hayo yalielezwa leo na Balozi  wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, ambapo amesema kuzinduliwa kwa mitandao miwili ya utafutaji ya Baidu,  utakuwa unatangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii (TTB).

Amesema pasipo na ndege ya uhakika kutangaza utalii inakuwa ni
changamoto kwani wachina wanapenda kwenda katika nchi ambazo zina
ndege za moja kwa moja kwa sababu wana tatizo la lugha.

Amesema Tanzania inafahamika katika masuala ya utalii kwa
upande wa Serengeti na Ngorongoro lakini bado kuna maeneo mengine
hayajafahamika hivyo yanahitajika kutangazwa na kwamba mtandao wa Baidu unatumika China na nchi nyingine duniani, hivyo itaitangaza nchi na watu wengi kuona utalii wa Tanzania.

Mhadhiri wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari ya
China, Maria Lee amesema kutangaza vivutio katika mtandao huo wa Baidu itasaidia kufahamika kwa utalii uliopo Tanzania ili Wachina wahamasike kuja kuvitembelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles