25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya wahadhiri wenye PhD yaongezeka DUCE

Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) kimesema idadi ya wahadhiri wenye Shahada ya Uzamili (PhD), walioajiriwa imepanda kutoka watatu mwaka 2005 hadi kufikia 80 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya utafiti chuoni hapo, leo Jumatano Aprili 3, Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Dk. Julius Mbuna amesema pamoja na changamoto mbalimbali chuo kinahakikisha wataalamu wanaotoka masomoni wanapata ofisi ili kuboresha shughuli za utafiti.

“Katika wiki hii, chuo kitaonyesha badhi ya miradi itakayoshindanishwa ili kupata washindi watatu watakaopata fedha taslimu na washindi watashindanishwa na washindi wengine katika maadhimsho hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yatakayofanyika Mei, mwaka huu,” amesema.

Hata hivyo, Mbuna amesema chuo hicho kipo katika hatua mbalimbali za kupitia sera ya utafiti pia kuendelea kudumisha na kuanzisha mahusiano mapya na vyuo na asasi nyingine ndani na nje ya nchi ili kutafuta mianya ya kushirikiana katika utafiti ambapo mpaka sasa chuo kina mahusiano na taasisi 23 kutoka karibu maabara zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles