31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya vifo yafikia 832 Indonesia

 Palu, Indonesia

Watu 832 wamefariki baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kupiga kisiwa cha Indonesia cha Sulawezi.

Kwa mujibu wa Shirika la Majanga la Kitaifa, juhudi za kutafuta miili ya watu hao zinaendelea na idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka maradufu kutokana na maeneo mengi hadi sasa hayajafikiwa na waokoaji.

Shirika hilo limesema eneo lililoathiriwa ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa. Watu wengine waliripotiwa kukwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomka siku ya Ijumaa.

Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata sita ambapo sehemu kubwa ya Mji wa Palu, imeharibiwa vibaya huku dalili za kuwapata walionasa wakiwa hai zikianza kufifia.

Katika ziara yake kwenye mji wa Palu, Rais wa Indonesia, Joko Widodo, amewaambia viongozi wa eneo hilo kuwa serikali kuu itatoa mahitaji yote muhimu ili matengenezo mapya ya mji huo yafanyike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles