29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya vifo vya corona yaziri kupaa

Beijing, China

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya corona imeongezeka na kufikia zaidi ya 1,000 wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likionya kuwa watu walioambukizwa na hawajasafiri kwenda China huenda wakawasha moto mkubwa katika janga hilo.

Ongezeko la vifo limekuja baada ya Rais Xi Jinping kufanya ziara isiyo ya kawaida katika hospitali moja ya Beijing, akiwa amevaa vifaa vya kujikinga, na kushauriana na wahudumu wa afya na wagonjwa.

Timu ya mwanzo ya ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na WHO imewasili China, wakati nchi hiyo ikipambana kudhibiti virusi hivyo vilivyoambukiza zaidi ya watu 42,000 na kusambaa hadi nchi 25.

Vifo vingine 108 viliripotiwa jana, wakati Serikali ya China ikiwazuia mamilioni ya watu katika miji kadhaa.

Serikali kadhaa za kigeni zimepiga marufuku watu kuwasili kutoka China na mashirika makubwa ya ndege yamesitisha safari ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Jana, Shirika la habari la BBC lilieleza kuwa katika harakati za kukabilina anugonjwa huo, mkongwe wa filamu nchini China, Jackie Chan ametangaza rasmi kupitia mtandao wa Weibo kuwa atatoa fedha kwa ajili ya mtu yoyote atakayegundua kinga ya ugonjwa wa corona.

Chan aliweka wazi kiu yake ya kutaka kumaliza kabisa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa corona kwa kutangaza kutoa zaidi ya Dola za kimarekani 140,000 kwa mtu ama kikundi kitakachofanikisha kugundua kinga dhidi ya ugonjwa wa corona.

Virusi vya corona ni hatari kiasi gani?

Watu zaidi ya 75,000 wanaweza kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, katika mji wa Wuhan, wataalamu wameeleza.

Ingawa makadirio ya chuo kikuu cha Hong Kong yanasema kuwa inawezekana kuwa idadi ikawa kubwa zaidi ya takwimu zinazotajwa rasmi.

Ripoti zinasema kuwa kuna watu ambao walifariki wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo ulipoanza tu, jarida la afya la Lancet linasema kuwa wagonjwa wengi walikufa bila kufahamika kile kilichowauwa.

Ripoti imebaini kuwa wagonjwa 99 walihudumiwa katika hospitali ya Jinyintan huko Wuhan , 40 kati yao walikuwa na magonjwa ya muda mrefu kama magonjwa ya moyo au presha, wengine 12 walikuwa wana kisukari.

Zuio la watu kusafiri linasaidia?

“Katazo la watu kusafiri linasababisha watu kuingia kwenye matatizo zaidi, kwa sababu watu wanakosa taarifa, usambazaji wa madawa unakuwa duni, uchumi unashuka na hata watu wanatafuta njia ambaozo si rasmi kuondoka katika eneo lililoathirika, mkuu wa shirika la afya alisema siku ya Ijumaa.

Hali ya maambukizi hivi sasa ipoje?

Ingawa virusi vimesambaa mpaka nje ya China, kukiwa na ripoti ya maambukizi kwenye mataifa 25, mpaka sasa kumeripotiwa vifo viwili nje ya China- mtu mmoja Hong Kong na mtu mmoja Ufilipino.

WHO limetangaza mlipuko wa virusi vya corona kuwa janga la kiafya, likisema ikiwa fedha hazitaelekezwa kupambana na mlipuko, mataifa yatajutia hilo baadae.

Ingawa takwimu rasmi nchini zinasema kuna maambukizi 31,000, baadhi ya wanasayansi wamekisia kuwa idadi inaweza kuwa mara 10 zaidi, kwa kuwa wengi wao huonyesha dalili polepole, na hawapati matibabu, na hivyo kuwaambukiza wengine.

AFP, BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles