23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Idadi ya vifo vya corona yafikia 100,276

 WASHINGTON, MAREKANI

IDADI ya wagonjwa waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani imepita 100,000 katika kipindi cha chini ya miezi minne.

Taifa hilo limeandikisha vifo vingi zaidi ya taifa lolote lile huku watu milioni 1.69 wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo idadi ambayo ni asilimia 30 ya maambukizi yote duniani.

Maambukizi ya kwanza nchini Marekani yaliripotiwa mjini Washington Januari 21, 2020.

Kote duiniani kumekuwa na watu milioni 5.6 walioambukizwa virusi hivyo huku idadi ya vifo ikifikia 354,983 tangu mlipuko wa virusi hivyo kuzuka mjini Wuhan nchini China mwisho wa mwaka jana.

Kufikia sasa idadi ya waliofariki nchini Marekani imefikia 100,276, kulingana na Chuo kikuu cha John Hopkins mjini Maryland ,ambacho kimekuwa kikifuatilia mlipuko huo.

Muhariri wa BBC katika eneo la Marekani ya Kaskazini, Jon Sopel alisema kwamba idadi hiyo ni sawa na idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita vya Korea, Vitenam, Iraq na Afghanistan katika kipindi cha miaka 44 wakipigana.

Hata hivyo, Marekani imeoredheshwa ya tisa duniani kwa kiwango cha watu wanaofariki nyuma ya Ubelgiji, Uingereza , Ufaransa na Ireland kulingana na chuo hicho.

Majimbo 20 yaliripoti kuongezeka kwa kesi mpya kwa wiki iliokuwa inaisha siku ya Jumapili, kulingana na utafiti wa Reuters.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles