29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hukumu kwa anayedaiwa kumuua Mwangosi Julai 21

Daudi Mwangosi
Marehemu Daudi Mwangosi

NA Raymond Minja, Iringa

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa,imesema Julai 21,mwaka huu itatoa hukumu ya   polisi Pasificus Cleophance Simon anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na mwakilishi wa kituo cha Chanel Ten, marehemu Daudi Mwangosi.

Kabla ya kutoa uamuzi huo, Jaji   Paul Kiwelo alisema, “Leo (jana) ni siku ya kusikiliza majumuisho ya kesi hii inayomkabili mtuhumiwa Pasificus Cleophance Simon aliyeko kizimbani, nawashukuru mawakili wote wa pande mbele kwa  kazi kubwa mliyofanya.

“Leo (jana) ni siku ya wazee wa baraza kutoa maoni yao na ushauri wenu juu ya kesi hii na kumbukeni kesi hii ni kubwa inayogharimu maisha ya mtu,matumaini yangu mtafanya kazi yenu kwa weledi uliotukuka ”

Baada ya kusoma majumuisho ya kesi hiyo kutoka mwanzo hadi mwisho,Jaji Kiwelo aliwapa nafasi wazee wa baraza kutoa maoni yao juu ya kesi hiyo, lakini wazee hao waliomba muda wa dakika 15   kupumzika kidogo na kujadiliana nje.

Akitoa maoni yake juu ya kesi hiyo, mzee wa mahakama Hadija Husseni alisema kutokana na ungamo lililowakilishwa mahakamani hapo kutoka kwa mlinzi wa amani, mtuhumiwa alikiri kwa maandishi na kutia saini yake kuwa yeye ndiye aliyehusika na kifo cha mwandishi wa habari Mwangosi.

Alisema  kwa ungamo hilo ambalo mtuhumiwa alitoa akiwa huru na amani inaonyesha kuwa mtuhumiwa ana kosa la kumuua Daudi Mwangosi bila ya kukusudia.

Mzee mwingine wa mahakama, Saidi Mbaga alisema  kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hakuna ushahidi wowote unaomhushisha mtuhumiwa moja kwa moja kuwa alimuua Mwangosi,hivyo mtuhumiwa hana hatia.

Alisema  shahidi Mwinuka katika maelezo yake yeye akiwa ni msimamizi wa kazi iliyokwenda kufanyika Mafinga,shahidi huyo alikiri kutomuona mtuhumiwa

akitenda kosa hilo.

Alisema  pia shahidi namba mbili, Mwampamba aliyetoa ushahidi wake mahakamani juu ya kilichotokea eneo la tukio,alitoa maelezo ya kuambiwa na watu kwa kuwa baada ya tukio hilo kutokea shahidi alipata mshituko na kuzinduka siku ya pili.

Alisema kutokana na hali hiyo, yeye hawezi kuthibitisha kama mtuhumiwa alitenda kosa hilo zaidi ya kuona picha kwenye gazeti ambayo pia inadhaniwa siyo ya mtuhumiwa.

Hata hivyo, Mbaga alisema shahidi wa mwisho PC Lewisi alipotoa ushahidi wake   hakuna sehemu inayomuonyesha shahidi akitaja silaha aliyotumia mtuhumiwa kumuua Mwangosi.

Naye Sophia Nganguli alisema  ushahidi uliotolewa na Jamhuri umeacha shaka nyingi kwa kuwa baadhi ya ushahidi waliotoa walishindwa kuthibitisha moja kwa moja kuwa mtuhumiwa alihusika kumuaa Mwangosi.

Licha ya kutoa maelezo hayo, N’ganguli alisema mbali na Jamuhuri kuonyesha ushahidi wao una shaka,lakini kutokana na ungamo ambalo mtuhumiwa alilitoa mbele ya mlinzi wa amani  kwa kukiri kosa tena kwa kusikitika (nasikitika sana kusababisha kifo cha Mwangosi), inaonyesha wazi alitenda kosa hilo.

Baada ya wazee hao wa baraza   kutoa maoni yao kwa jinsi walivyoona mwenendo mzima wa kesi na kuzingatia ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na pande zote mbili, Jaji Kiwelo aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 21, mwaka huu siku ambayo atatoa hukumu.

Kwa mara ya kwanza, mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani Septemba 12, 2012 akituhumiwa kumuua Mwangosi kwa kukusudia katika tukio lilitokea Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa Septemba 2,2012 wakati mwandishi   alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles