MKUMBO AWAOMBA WADAU MAONI SHERIA YA MAJI

0
488

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


KATIBU Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewaomba wadau wa maji nchini kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusiana na utungaji wa sheria mpya ya maji

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa menejimenti mpya katika ofisi za Dawasa jijini Dar es Salaam jana Profesa Mkumbo amesema kuwa sheria hii mpya itasaidia mambo mengi ikiwa ni pamoja na udhibiti wa maji ambayo yamekuwa yakipotea kwa asilimia 44 mpaka sasa.

Alisema wizara inapendekeza kuanzishwa kwa Taasisi maalumu  ya kushughulikia miradi ya maji mijini na vijijini yaani Rural Water Agency.

“Taasisi hiyo imekusudia kuimarisha Jumuiya za watumiaji wa maji kwa ngazi za vijiji na mijini ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa Taasisi mpya ya Dawasa,” alisema Profesa Kitila.

Alisema kutungwa kwa sheria mpya ya maji kutaongeza matamanio kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi kwa uhakika.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja aliwataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kishirikiana na Dawasa katika ufanyaji kazi wake hasa kutoa taarifa punde inapobainika uvujaji wa maji.

Alisema utungaji wa sheria mpya unapofanyika wananchi watoe maoni ili mchakato uwe na tija kwani sheria hii ina manufaa makubwa kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here