33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Rufaa Simiyu yajiandaa kuanza upasuaji mkubwa

Na Derick Milton- Simiyu

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambayo kwa sasa inatoa huduma za wagonjwa wa nje tu, itaanza rasmi kutoa huduma za upasuaji mdogo na mkubwa Novemba.

Akongea na MTANZANIA Ofisini kwake jana, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Matoke Muyenjwa, alisema tangu hospitali hiyo imeanza kufanya kazi baada ya kuzinduliwa na Rais John Magufuli mwaka mmoja umepita ikiendelea kutoa huduma.

“ Wananchi wameendelea kuteseka na kutumia gharama kubwa kufuata huduma hizo mkoani Mwanza na mikoa mingine, baada ya majengo yetu kukamilika ya maabara, mionzi na upasuaji, tutatoa huduma hizo hapa hapa.

 “ Tunawahakikishia wananchi wa mkoa wa wetu hospitali hii inaenda kuwa mkombozi kwao na kuwapunguzia gharama, Novemba tunaanza rasmi, tayari tumeanza maandalizi ya vifaa tiba vyote vinavyohitajika zikiwemo mashine za upasuaji mkubwa na madaktari bingwa wapo wa kutosha,” aliongeza Dk Myunjwa.

Alisema ujenzi wa majengo hayo upo katika hatua za mwisho, ambapo alisema wamedhamiria hospitali hiyo kutoa huduma za kibingwa kutokana na kuwepo kwa madaktari bingwa wengine wanaoamaliza masomo yao.

“Kuanza kutolewa kwa huduma za upasuaji mkubwa na mdogo, itapunguza kwa zaidi ya nusu ya rufaa za wagonjwa kwenda Hospitali ya Bugando, tunao madaktari wa kutosha na wenye uzoefu lakini wapo wauguzi zaidi ya 60,” alisema Dk Muyenjwa

Aidha alieleza kuwa katika kuazimisha mwaka mmoja wa hospitali hiyo tangu kuanza kazi, walifanya kampeini ya kutoa huduma za vipimo vya virusi vya homa ya ini na magonjwa yasiyoambukizwa.

Alisema katika huduma watu 257  walipimwa magonjwa mbalimbali huku 33 wakipimwa virusi vya homa ya ini na mmoja kati hao kukutwa na virusi hivyo na 60 wakikutwa na tatizo la uzito uliopitiliza.

Janeth John mmoja wa wananchi walioshirikia zoezi hilo, aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa vipimo na ushauri, ambapo alisema imesababisha atambue tatizo lake na kupewa ushauri na dawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles