25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Bugando yaokoa Sh bilioni mbili kwa wananchi

Na Mwandishi wetu-Mwanza

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC), imeokoa Sh bilioni mbili kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa kusafiri kwenda Dar es Salaam kupata tiba ya saratani kila mwaka.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi, wakati akizungumza na maofisa habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake, waliokuwa Mwanza kujionea mafanikio ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Profesa Makubi alisema kuanza kwa tiba ya saratani katika Hospitali ya Bugando, kumesaidia kuokoa fedha hizo kutoka kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa ambao awali walilazimika kwenda Dar es Salaam kupata huduma hizo Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

 â€œTunaishukuru Wizara ya Afya ambayo ilitupatia Sh bilioni 5.5 ili kujenga jengo la saratani. Kama hospitali tumeweza kununua mashine nne za mionzi na dawa kwa kushirikiana na wafadhili wengine,” alisema Profesa Makubi.

Alisema kwa sasa asilimia 90 ya wagonjwa wa kanda hiyo wanapata huduma katika hospitali hiyo, hivyo kuwaondolea adha ya kusafiri kupata huduma mbali.

Mtaalamu wa Tiba Mionzi wa Idara ya Saratani ya BMC, Alex Mpugi, alisema kabla ya mashine hizo walikuwa wakitoa huduma za saratani kwa kutumia kemikali.

“Naomba nitoe wito kwa wananchi, hususan wanawake  kujitokeza kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti kila siku ya Jumanne na Alhamisi,” alisisitiza Mpungi.

Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk. Fabian Massaga, alisema hospitali imefanikiwa kufanya ukarabati na upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka sita hadi 13 ambavyo viwili hutumika kwa upasuaji wa dharura na kimoja kwa upasuaji kwa wajawazito.

Dk. Massaga alisema upanuzi huo umeendana na ununuzi wa vifaa vipya na vya kisasa, ikiwemo vitanda vya kufanyia upasuaji, taa maalumu za vyumba vya upasuaji na mashine za kisasa za kutolea dawa ya usingizi.

Alisema vifaa hivi vimeagizwa moja kwa moja viwandani kwa takribani Sh bilioni 1.4 badala ya Sh bilioni 3 kama wangenunua kwa wauzaji hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles