Hofu yatanda mwandishi aliyetoweka Uturuki

0
547
Jamal Khashoggi

ISTANMBUL,Uturuki

HOFU  inazidi kuongezeka kufuatia kutoweka kwa mwandishi wa habari nchini hapa,  Jamal Khashoggi baada ya maofisa wa serikali kusema wanaamini ameuawa.

Khashoggi, ambaye ni raia Saudi Arabia alitoweka baada ya kuingia ubalozi wa nchi hiyo uliopo mjini hapa mwanzoni mwa wiki hii.

Afisa mmoja wa hapa aliliambia Shirika la Utangazji la Uingereza BBC kuwa uchanguzi wa awali ulionyesha kuwa aliuawa akiwa ndani ya ubalozi huo madai ambayo yanakanushwa na Saudi Arabia ikisema kwamba  imeanza kumtafuta.

Mwandishi wa BBC mjini aliyepo mjini hapa, Mark Lowen, alisema hii itachangia uhusiano kati ya Saudi Arabia na Uturuki kuwa mbaya zaidi.

Alisema kwamba maofisa wa serikali ya hapa  wameanzisha uchunguzi na wamekuwa wakizungumza na vyombo vya habari, lakini  hawajatoa ushahidi kwa madai yao, wala kueleza ni jinsi gani aliuawa.

Jamal Khashoggi ni mkosoaji mkubwa wa mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman na ana zaidi ya wafuasi milioni 1.6 katika mtandao wake wa  Twiter na analifanyia kazi gazeti la the Washington Post .

Inaelezwa kuwa wakati akitoweka siku ya Jumanne alikuwa kwenye ubalozi kupata hati  za  kumtaliki mke wake wa zamani ili apate kufunga ndoa na mchumba wake raia wa hapa,  Hatice Cengiz.

Mchumba wake huyo alisema  Khashoggi alihitajika kusalimisha simu yake ambayo ni sheria kwenye balozi nyingi na  aliambiwa ampigie simu mshauri wa Rais Recep Tayyip Erdogan ikiwa hangerudi kutoka ubalozi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here