27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu ya corona yamfanya ajifungie ndani miezi mitano sasa

NKa AVELINE KITOMARY

KATIKA kipindi hiki ambapo Dunia imekuwa ikiathiriwa na mlipuko wa homa kali ya mapafu

inayosasababishwa na virusi vya corona (Covid-19), hofu kubwa imetanda kwa watu ambao tayari wanamagonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Hii inatokana na uthibitisho wa wataalamu wa afya kusema kwamba virusi vya corona vina nafasi kubwa zaidi kumshambulia na kumwathiri mtu ambaye kinga zake za mwili ni dhaifu.

Moja ya kundi ambalo liko hatarini zaidi endapo watapata virusi vya corona ni wagonjwa wanaoungua ugonjwa wa lupus, hii ni kwa sababu tayari kinga zao ziko katika mfumo wa to- fauti.

Lupus ni ugonjwa unaotokea pale ambapo kinga za mwili huacha kazi yake ya kulinda mwili na badala yake kushambulia kwa kuonesha uharibifu katika sehemu mbalimbali za mwili kama ngozi, figo na mapafu.

Ugonjwa huu pia unatabia ya kujificha kwenye magonjwa mengine hasa unaposhambulia mapafu, huweza kudhaniwa kama Kifua Kikuu (TB), hali hiyo husababisha wagonjwa hao kupewa dawa za TB.

Ni rahisi zaidi wagonjwa hawa kupata maambukizi ya ma- gonjwa mengine, hii ni kutokana na miili yao kutokuwa na kinga ya kutosha.

Kwa mujibu Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk. Francis Furia, lupus ni ugonjwa unaoshambulia zaidi watu weusi hasa wanawake.

Dk. Furia ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Figo, anasema ni muhimu wagonjwa wa lupus kujilinda wakati wote kutokana na urahisi wa kupata maambukizi.

“Kama tunavyojua, kwa kawaida kazi ya jeshi ni kuilinda nchi ili maadui wasiivamie pale ambapo jeshi linapoacha kazi yake ya kuilinda nchi na kuanza kuishambulia, hii ndio maana halisi ya ugonjwa wa lupus.

“Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu mabalimbali za mwili, ndio maana unaitwa ‘systematic Erythematosus disease’ unatokea baada ya kinga za mwili kuanza kushambulia mwili, kama tunavyojua kazi ya

kinga za mwili ni ulinzi lakini zinapogeuza kazi zake huwa hatari,” anaeleza Dk. Furia.

Anasema hakuna utafiti wa kisanyasi unazothibitisha sababu za hali hiyo kutokea.

“Utafiti unasema ugonjwa huo unawaathiri zaidi watu weusi hasa barani Afrika, ukienda nchi za Ulaya wanaopata pia ni watu weusi.

“Asilimia kubwa ya wanaoathirika ni wanawake, katika kila watu 20 anayepata ni mwanaume mmoja, huku idadi ya watu wazima ikiwa kubwa zaidi kuliko watoto.

“Tafiti bado zinaendelea kufanyika kubaini chanzo cha ugonjwa huo ila inahusishwa pia na miale ya jua, hali ya hewa lakini hakuna uthibitisho wa hilo hata vinasaba vinahusishwa pia,” anabainisha Dk. Furia.

Anasema kuwa utafiti wa Muhimbili wa kuanzia mwaka 2012 hadi 2018 ni watoto wanne pekee waliopatikana na ugonjwa huo.

Hivyo, hayo ni magonjwa yanayotokea kwa watu wachache huku tafiti za kidunia zikinaonesha kwamba kuna wagonjwa 20 hadi 150 kwa kila watu 100,000.

CORONA YAMUWEKA NDANI MIEZI MITANO

Hajrrath Mohammed, ni msichana mwenye umri wa miaka 25 anayesumbuliwa na ugonjwa wa lupus, anasimulia jinsi ambavyo mlipuko wa ugonjwa wa corona ulivyobadilisha maisha yake.

Hajrrath anasema ni miezi mitano sasa hajatoka nje ya nyumba yao tangu ugonjwa wa corona kuanza kuripotiwa na kutajwa kuongezeka kwa kasi duniani.

Sababu kubwa inayomfanya kukaa ndani ni hofu ya kuweza kuambukizwa virusi hivyo.

Anasema amekuwa akikaa katika chumba chake ambapo mtu yeyote hawezi kuruhusiwa kuingia isipokuwa anayechukua tahadhari za kiafya.

“Duniani kote wagonjwa wa lupus katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa corona tunashauriwa kukaa ndani, tangu January hadi sasa sijatoka nje kutokana na kuhofia kupata maambukizi ya virusi vya corona.

“Ninakaa katika chumba changu peke yangu sitoki hata katika familia yangu sichangamani na watu wengine kabisa kutokana na wengine kutoka nje, kwani ninaweza kuletewa virus

nyumbani na kama nikiletewa chakula anayeleta anahakikisha amefuata tahadhari zote za kiafya.

“Ninafanya hivi sio kwa sababu ninapenda bali ni kutokana na hali yangu kiafya, kama inavyojulikana sisi wagonjwa wa lupus kinga zetu za mwili ni dhaifu hivyo, ikitokea kuwa umepata virusi vya corona hali inaweza kuwa mbaya zaidi hata kupoteza maisha,” anasimulia Hajrrath.

Licha ya wataalamu wa afya kuwataka watu kuchukua tahadhari mbalimbali za kiafya, ikiwamo kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa ‘mask’, kuepuka mison- gamano na tahadhari zingine, Hajrrath anasema tahadhari hizo huenda zisiweze kumsaidia.

“Kama nilivyosema mwanzokuwa uwezo wa kupata haraka virusi hivyo ni mkubwa wakati mwingine unaweza kunawa mikono na ukaja kuambukizwa kwa njia ya hewa tu hivyo, suluhisho ambalo mimi naona kwa wagonjwa wa Lupus ni kukaa ndani tu.

“Hata wenzangu nawasihi waendelee kukaa ndani kwa usalama wao, pia tuzingatie tahadhari za kiafya tunapokuwa nyumbani kwa sababu katika familia kuna watu wanatoka na kuingia hivyo muda mwingi kaa chumbani peke yako, usiruhusu mtu kuingia ndani ya chumba chako kiholela.

AELEZA SHUGHULI ZAKE ZILIVYOATHIRIKA

Hajrrath ambaye pia ni Mwe- nyekiti wa Chama cha Lupus Awareness and Support Faundation (LASF), anasema licha ya kutafuta ajira kwa muda mrefu na kukosa, shughuli kubwa anayofanya kupitia taasisi hiyo ni kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa lupus.

Anasema mara nyingi amekuwa akifanya kampeni katika maeneo mengi ya jiji la Dar
es Salaam na nje ya jiji hilo, ili jamii kuweza kuelewa ugonjwa huo na kuacha unyanyapaa kwa wagonjwa hao.“Tangu nilivyo- jifungia ndani sijapata tena njia ya kuweza kuwasiliana na jamii, siwezi tena kuendelea kutoa elimu licha ya kuwa tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo unyanyapaa, mitazamo hasi kuhusu ugonjwa huu, changano- to za ajira na mengineyo.

“Kwa upande wa mitazamo, wapo wanaochukulia lupus kama ushirikina, wengine wanasema saratani ya ngozi, mkanda wa jeshi na wengine Ukimwi kwahiyo, kunahaja jamii kujengewa uelewa,” anaeleza.

Kwa mujibu wa Hajrath, katika jamii wapo watu wanaoteng- wa na kubaguliwa kutokana na ugonjwa hasa wale ambao ngozi zao zimeathiri.

“Wakati mwingine wagonjwa wanaposhindwa kumudu hali ya unyanyapaa hujaribu hata kujiua, hata mimi mwanzoni nilikuwa najaribu kujiua kuto- kana na maumivu makali na ngozi kubadilika, nilikuwa hata nikitembea nahisi maumivu.

Anasema changamoto zingine ni wagonjwa hao kukosa ajira kutokana na hali yao ya kiafya kubadilika mara kwa mara.

“Hadi leo hii sijapata kazi, niliamua kujiajiri kwa kufanya biashara ndogondogo, ukiwaambia watu hii ni lupus hawaamini kabisa wanakunyima ajira, hivyo elimu inahitajika zaidi kwa sababu ugonjwa huu unawapata watu wachache,” anasisitiza Hajrrath.

DAKTARI ANENA

Akizungumzia kuhusu mitazamo ya jamii kuhusu ugonjwa huo, Dk. Furia anasema huenda ikawa sahihi kutokana na ugonjwa huo kushambulia se- hemu mbalimbali za mwili kama ulivyo Ukimwi.

“Wakati mwingine mapafu ya mgonjwa yanajaa maji hapo madaktari wengi wanajua ni TB kutokana na kukosa vipimo na karibu asilimia 50 ya wagonjwa wenye TB wanavirusi vya Ukimwi.

Anasema mgonjwa wa lupus anatakiwa kutumia dawa haraka kwani asipotumia uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa.

“Miaka mitano iliyopita tulikuwa hatuna vipimo sampuli zilikuwa zinatumwa nje ya lakini sasa tunavipimo na dawa zipo pia.

“Tiba ya ugonjwa huu ni dawa ambazo zinapunguza kiasi cha ukubwa wa kinga za mwili hizo dawa kwa kitaalamu zinaitwa ‘Immurosuppressants’ pia wapo madaktari wawili tu hapa nchini wanaotibu ‘Rheumatic condi- tion’ na wanaitwa ‘Rheumatolojist.’ Gharama za dawa zinatofautiana kutokana na sehemu mgonjwa alipoathirika, kuna kidonge cha Sh 6,000 hadi Sh 60,000,” anabainisha Dk. Furia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles