25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hillary: Urusi inaandaa mgombea wa Democrat kumsaidia Trump

NEW YORK, MAREKANI

MGOMBEA wa zamani wa chama cha Democrat nchini Marekani, Hillary Clinton amesema kwamba Urusi inamuandaa mgombea wa kike wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa 2020.

Amesema kwamba taifa hilo linataka mgombea huyo kuwania kama mgombea wa tatu ili kugawanya kura na kusaidia kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump.

Hillary hakumtaja mgombea huyo, lakini anaaminika kuzungumzia kuhusu mbunge Tulsi Gabbard. Gabbard alidaiwa kutaja madai ya Hillary kama ya ‘uoga’.

Katika mahojiano na makao makuu ya mshauri wa rais wa zamani, Barrack Obama David Plouffes, Hillary ambaye yeye mwenyewe ni mwanachama wa Democrat alisema kwamba Urusi inamlenga mtu ambaye kwa sasa anaendelea na kampeni zake na kwamba wanamuandaa kuwa mgombea wa tatu.

“Anapigiwa upatu na Urusi,” Hillary alisema, bila ya kumtaja. Wana mitandao chungu nzima na njia nyengine za kumuunga mkono kufikia sasa.

Hata hivyo, Gabbard alijibu akimshutumu Hillary kwa kuanza kampeni za kumharibia sifa yake.

Alimpatia changamoto mgombea huyo wa zamani kujiunga katika kinyanganyiro cha Ikulu badala ya kujificha nyuma ya wengine.

Gabbard ni mwanajeshi mkongwe na mgombea ambaye ameitaka Marekani kutojifanya kama polisi wa duniani.

Katika mjadala wa moja kwa moja akishirikiana na wagombea wengine 11 siku ya Jumanne, alisema kwamba madai ya vyombo vya habari vya Marekani kwamba anasukumwa na Urusi hayafai hata kidogo.

Hillary pia alimshutumu mgombea wa chama cha Green Party, Jill Stein kwa jina kwa kuwa msaliti.

Alizua uwezekano wa kwamba Stein anaweza kugombea kama mtu wa tatu kwa kuwa pia naye anasukumwa na Urusi.

“Ni kweli yeye anatumika na Urusi, namaanisha kabisa. Wanajua kwamba hawawezi kushinda bila kuweka mgombea wa tatu,” aliongezea Hillary.

Idadi ya kura alizopigiwa Stein katika majimbo matatu ambayo yalijitokeza yalikuwa muhimu kwa matokeo yote kwa jumla, Michigan, Pennsylvania na Wisconsin – zilizidisha ushindi wa Trump dhidi ya Hillary.

Hata hivyo kuna mjadala kuhusu iwapo Stein alisaidia katika uchaguzi wa Trump kwa kuwa data zinasema kwamba sio wapiga kura wote wa Stein wangempigia kura Hillary ama chaguo lao la pili ama hata kupiga kura kabisa.

Stakhabadhi kutoka kwa uchunguzi wa wakili maalum, Robert Mueller unaonyesha kwamba raia wa Urusi na mshirika walifanya kazi kuimarisha kampeni ya Stein katika juhudi ya kuchukua kura kutoka kwa Hillary.

Mwaka 2018 , Stein alitambua hatua ya rais kuingilia kati uchaguzi wa Marekani lakini akaongezea kwamba Marekani pia iliingilia uchaguzi ughaibuni.

“Kuingilia uchaguzi ni makosa na ni shambulio dhidi ya demokrasi na kwamba suala hilo linafaa kufuatiliwa” aliambia CNN.

Lakini Marekani inapaswa kulichukulia kana kwamba inalijua jambo hilo.

Mgombea wa chama cha Green Party Ralph Nader mwaka 2000 alilaumiwa katika ikulu ya Whitehouse kwa kumsaidia George W Bush , kutoka chama cha Republican , kupata ushindi katika jimbo la Florida na hivyo basi Urais wa Marekani kwa Jumla.

Siku ya uchaguzi iko zaidi ya mwaka mmoja ujao lakini ushindani wa kuwa mgombea wa Democrat dhidi ya Trump tayari umeanza.

Kura ya maoni inasema kwamba Warren na Joe Bidden ndio wagombea walio kifua mbele huku Sanders akiwa mgombea maarufu pia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles