30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HESABU ZA YANGA MAPINDUZI ZAGOMA

NA SAADA AKIDA-UNGUJA


HESABU  za Yanga kufuzu fainali na hatimaye kutwaa ubingwa wa  Kombe la Mapinduzi zimegoma baada ya jana kuchapwa penalti 5-4na URA katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan,Unguja.

Katika mchezo huo,timu hizo zilikamilisha dakika 90 bila kuruhusu nyavu za kila mmoja kutikishwa,ndipo kanuni ya mikwaju ya penalti ilipotumika kumsaka mshindi.

Waliofunga penalti kwa upande wa Yanga ni Raphael Dauni,Hassani Ramadhan,Gadiel Michael na Papy Tshishimbi,huku Obrey Chirwa akikosa baada ya penalti yake kudakwa na kipa wa URA,Alianzi Nafian.

Kwa upande wa URA waliopiga  penalti na zote tano walikua, Bakota Labama, Kibumba Enock, Kaenmu Shafik, Kulaba Jimmy na Majgwa Brian.

 

Mara baada ya mchezo huo,URA ilionekana kucheza kwa kasi na kushambulia lango la Yanga mara kwa mara

Dakika ya pili,kiki ya  Nicholas Kagaba ilitoka nje kidogo ya lango la Yanga.

URA ilifanya shambulizi jingine dakika ya 13,ambapo kiki kali ya Julius Mutyaba ilitoka nje la lango la Yanga.

Yanga ilijibu dakika ya 35,ambapo mpira wa adhabu wa Ibrahim Ajib ulipaa juu ya lango la URA.

Daika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika  kwa timu kutofungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kucheza kwa tahadhari kila moja ikiohofia  kuruhusu bao.

Yanga ilifanya mabadiliko dakika ya dakika ya 53,alitoka Pius Buswita na nafasi yake kuchukuliwa na Obrey Chirwa.

Hata hivyo,mabadiliko hayo yalionekana kuidhoofidha Yanga badala ya kuiongezea nguvu  kwani Chirwa alionekana kutokuwa fiti kiasi cha kutosha  hatua iliyosababisha  kuharibu mipango ya timu yake.

 

URA ilifanya mabadiliko dakika ya 69, alitoka Bakota Labama na kuingia Lwasa Peter,pia alitoka Ssempa Charles na kuingia Mulikyi Hudu.

Kuona hivyo,Yanga ilifanya mabadiliko kwa mara nyingine,dakika ya 75 alitoka Juma Mahadhi na kuingia Yohana Mkomola.

Dakika ya 77,kiki ya Ibrahim Ajib ilionekana nyanya kwa kipa Alionz Nafian wa URA.

Dakika ya 81 kilizuka kizaa zaa baada ya wachezaji wa URA kumvaa mwamuzi Issa Haji wakitaka akubali bao lao,ili hali mpira uliopigwa na mchezaji mwenzao,Lwasa Peter  ulipenya katika nyavu ndogo na kujaa kimini.

 

Sekeseke hilo lilisababisha  mwamuzi huyo kumlamba  kadi ya njano, Kagaba Nicholas kutokana na kupinga  maamuzi yake.

Ikionekana kudhamiria kutaka ushindi,URA ilifanya mabadiliko mengine dakika ya 90,alitoka Kalama Debosi na kuingia Kulaba Jimmy,Yanga ilijibu kwa kumtoa ,Juma Makapu na kuingia Raphael Daud.

 

Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kubadili matokeo hadi kipyenga cha kuashiria kumalizika kwa dakika tisini kilipopuliza na timu hizo kwenda kwenye mikwaju ya penalti na kushuhudiwa URAwakiibuka wababe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles