26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hatua 10 za kukuwezesha kupandishwa cheo

NA DK. CHRIS MAUKI

WATU wengi hutamani sana kupandishwa vyeo baada ya kuchoka sana na nafasi walizokuwa nazo kwa muda mrefu, au pia wengine wanatamani sana kupandishwa vyeo kwasababu ya kuongeza kipato ili kufikia malengo fulani maishani, kila mmoja ana sababu binafsi ya kuhitaji kupandishwa cheo. 

Taarifa za kupandishwa cheo ni za kufurahisha kwa kila mmoja wetu, wako ambao kuilazimisha fursa hii hata kwa kwenda kwa waganga, kuhonga, kujipendekeza, kujitoa miili yao na njia nyingine nyingi ili tu kupata cheo. 

Mara nyingi tumejiuliza kwanini sipandi cheo, wengine wapya wanakuja hapa wanafanya kazi kidogo mara wanapandishwa cheo, wanabadilishiwa ofisi, wanapata gari la ofisi, nyumba, na marupurupu mengine lakini si mimi.

Ukweli ni kwamba sababu kubwa ni sisi wenyewe, vitu vinavyotuangusha na kutufelisha si vile vilivyo nje yetu bali vile vilivyo ndani yetu, yaani vilivyo ndani ya uwezo wetu. 

Leo unaweza kuamua kufanya jitihada binafsi za juu ya namna ya kuweza kupandishwa cheo.Yamkini wewe ni mmoja wa hawa ninaowazungumzia hapa ili uweze kujikwamua

Jaribu kufuata kanuni hizi rahisi:

1. Jitahidi kujuana na watu

Unaweza kufikiri kuwa njia pekee ya kubadilisha mazingira uliyo nayo ni kukaa na kuwaza sana, hapana, hii siyo kweli, jaribu kujipenyeza kufahamiana na wengine, usijitenge sana, shiriki maisha yako na wale walioko karibu nawe.

Usifikiri kuwa wewe hustahili kujichanganya katika mazungumzo ya kawaida na watu wa ofisini kwako, usifikiri kuongea na bosi wako masuala ya kawaida ni kujipendekeza, kumbuka kwa kuwajua na kujichanganya na wafanyakazi wenzako tunajenga nguvu ya umoja wa kazi, taratibu wote tunakuwa ni timu moja katika utendaji. 

Pia usibaki umefungiwa katika kiti chako au meza yako ya kazi hata zile nyakati ambazo wengine wanapumzika au kujiburudisha, kama kuna hafla ya ofisi na wenzako wanakwenda basi shiriki nao, usifikiri wanapoteza muda, kama mwenzako anatukio fulani la furaha nyumbani basi usiache kushiriki, na kama wewe una tukio kama hilo kwako basi wakaribishe wenzako na usisahau kumualika hata na bosi wako. Taratibu unapoanza kumfahamu zaidi bosi wako ni mwelekeo mzuri katika kuelekea mafanikio yako. 

2. Usijifanye mkamilifu katika kila kitu

Usije ukafikiri kuwa haukuumbiwa kufanya makosa, kufanya kosa kupo katika maisha ya mwanadamu. Kama wewe ni mtu unayefanya kazi sana si  kitu cha kushangaza sana ukikosea kitu. Ikiwa unatokea kufanya kosa, basi usikae ukijilaumu na kujiuliza kwanini umefanya kosa bali jifunze, pata somo katika kukosea kule na uendelee mbele. Kama utaweka akili yako yote katika kujichunguza kila kitu unachokifanya ili usikosee basi hata bosi wako anaweza kufikiri kuwa wewe ni kati ya wanaojifanya wakamilifu katika kila wafanyalo na kinyume chake cheo kikaenda kwa wenzako na si wewe. Usisahau kuwa waweza kujikuta unafanya vimakosa vingi zaidi wakati unajitahidi kujiweka mkamilifu katika jambo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles