Imechapishwa: Sat, Nov 11th, 2017

HARMONIZE, MKWEWE WAKUTANA ITALIA

Na CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKATI ya wiki hii, mkali wa Bongo Fleva, Harmonize aliungana na familia ya mpenzi wake, Sarah katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mrembo huyo iliyofanyika nyumbani kwao nchini, Roma, Italia ambapo alikutana na mzazi wa mpenzi wake huyo.

Staa huyo wa singo ya Shulala, alianza kuonyesha video na picha akiwa anapiga misele na mpenzi wake katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Roma ambapo baadaye usiku alijumuika na mkwe wake – mama Sarah katika chakula cha jioni.

“Tusidanganyike na anasa, tutambue kuna maisha baada ya ujana na mambo ya mjini. Wanasemaga fainali uzeeni, leo ndiyo kesho yako tamu ama chungu, simama katika njia yako fanya maamuzi,” alisema Harmonize akiwa kwenye picha ya pamoja na Sara pamoja na mkwewe.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

HARMONIZE, MKWEWE WAKUTANA ITALIA