HARMONIZE AWALIZA KINA MAMA KARIAKOO

0
386


IKIWA ni miaka mitano imepita tangu staa wa muziki Harmonize atoke kimuziki na kuachana na umachinga Kariakoo, Dar es Salaam, msanii huyo Jumatano hii aliibuka maeneo hayo na kugawa fedha kwa kina mama wanaouza matunda na wafanyabiashara ndogondogo.

“Usikate tamaa, hakuna aliyezaliwa tajiri au staa, hakuna kinachoshindikana, muhimu ni kupambana na hakuna kukata tamaa. Mimi nilishakuwa machinga hapa (Kariakoo) lakini leo nina afadhali,” alisema Harmonize akigawa fedha kwa kina mama ambao wengine walijikuta wanadondosha machozi ya furaha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here