27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Hapi akataa ombi la wananchi kumegewa ardhi ya Magereza

Francis Godwin -Iringa

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amekataa ombi la wananchi wa Kijiji cha Ikongosi wilayani Mufindi, la kuomba ardhi ya kulima ndani ya  eneo la Jeshi la Magereza.

Hapi alikataa ombi hilo jana, wakati wa mkutano wake wa kupokea kero za wananchi wilayani hapa.

Alisema ardhi ya Magereza ni kwa matumizi yake ya kuzalisha chakula kwa wafungwa.

Hapi alisema si kila ombi la wananchi watalitekeleza kwani kimsingi ardhi ya Magereza ni maalumu kwa utaratibu wa Serikali wa kuhifadhi ardhi kwa matumizi ya baadae.

“Serikali ina kawaida ya kuwekeza benki ya ardhi kwa ajili ya matumizi ya kijamii, ikitokea wananchi wameongezeka, Serikali inahitaji kujenga kituo cha afya ama shule, benki yake ya ardhi ndiyo hii iliyowekezwa kwenye taasisi zake,” alisema Hapi.

Alisema kama wakiruhusiwa kulima kwenye ardhi hiyo, itakuwa vigumu kuwaondoa pindi itakapohitajika kwa matumizi ya umma.

Hapi alisema iwapo wanahitaji eneo kwa ujenzi wa shule, wanaweza kukaa chini na Magereza ili kupewa eneo ila sio kwa kilimo.

Alisema kimsingi shule ni mali ya Serikali na Magereza ipo chini ya Serikali, hivyo wanaweza kupewa eneo la ujenzi na kuwekewa mipaka.

“Ila niwaeleze wazi wananchi kuwa sio kila ombi mnaloomba mnaweza kusikilizwa, maombi mengine hayawezekani, kama hili la kuomba ardhi ya Magereza kwa ajili ya kulima watu binafsi,” alisema Hapi.

Aliagiza Magereza kutumia wafungwa kuendeleza ardhi hiyo kwa kilimo kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.

Kuhusu mashamba ya bega kwa bega (ujamaa), yaliyotolewa enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwataka viongozi wa kijiji kuona sehemu ya ardhi iliyobaki kutenga kwa malisho ya mifugo kama ambavyo wananchi wanavyoomba.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wenye malalamiko kuhusu vitambulisho vya taifa na wana namba za Nida, kuendelea kutumia namba hizo kusajili laini zao za simu.

Mkuu wa Gereza la Isupilo, Benjamin Kabisa, alisema wamejipanga kulinda ardhi na kutekeleza agizo la rais la kuzalisha chakula kupitia wafungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles