30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hanspoppe: Sibabaishwi na wanaotumwa kutuvuruga

Zacharia Hanspoppe
Zacharia Hanspoppe

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe, amesema hababaishwi na presha za baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wanaotaka usajili wa wachezaji bora msimu wa 2016/17, kwa madai  kuwa  wanatumika kuvuruga  mipango ya usajili katika  klabu hiyo.

Kauli hiyo inatokana na kuvurugika kwa usajili wa mshambuliaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo ambaye alitarajiwa kutua Msimbazi hivi karibuni lakini inadaiwa kwamba alimalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dola 20,000 ambazo ni nusu ya fedha  walizokubaliana, huku kiasi kingine  walitarajia kumalizana akiwa nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Hanspoppe alisema kwamba, bado klabu hiyo ipo katika mchakato wa kuinasa saini ya mshambuliaji huyo  licha ya  baadhi ya mashabiki  kuwa vinara wa kuvuruga mpango huo.

“Suala la Mavugo bado linaendelea na likiwa tayari tutaliweka wazi, hao mashabiki waendelee tu kuwa  katika  presha  kwa maana ndio wavurugaji wakubwa wa mipango yetu ya usajili,” alisema Poppe.

Poppe alisema kwamba, bado klabu hiyo inaendelea na mipango ya kuboresha kikosi cha timu hiyo kwa kusajili wachezaji muhimu ili waweze kufanya vizuri msimu ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles