Hali ya hatari yatangazwa Sri Lanka

0
943

Serikali ya Sri Lanka imetangaza sheria ya hali ya dharura wakati wa usiku katika maeneo yote ya nchi, baada ghasia zilizoongozwa na Wakristo kuharibu misikiti na biashara zinazomilikiwa na Waislamu katika jimbo la Kaskazini Magharibi.

Polisi imesema sheria hiyo ilitakiwa kutekelezwa kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri leo Jumanne.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuyatawanya magenge ya ghasia katika sehemu kadhaa za jimbo hilo, katika siku ya pili ya vurugu dhidi ya Waislamu.

Maduka matatu yalichomwa moto katika mji wa Hettipola, na usiku wa kuamkia Jumatatu msikiti wa Abrar ulio katika mji wa Kiniyama ulishambuliwa.

Sri Lanka vile ile iliifunga kwa muda mitandao ya kijamii kufuatia ghasia hizo za Jumapili. Nchi hiyo imekuwa chini ya sheria ya hali ya hatari, tangu mashambulizi ya kigaidi ya siku ya Pasaka yaliyouwa watu zaidi ya 250 katika makanisa na mahoteli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here