25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Hakuna sabuni inayorejesha usichana’

Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

WATANZANIA wametakiwa kuwa makini na baadhi ya wazalishaji wa bidhaa matapeli wanaotangaza sabuni wanazozalisha zinarudisha usichana.

Tahadhari hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga, wakati akizungumza na MTANZANIA jijini Mbeya jana.

Alisema kuna sabuni zimekuwa zikitangazwa na kuandikwa kwenye vifungashio kuwa zinarudisha usichana (bikra) kwa wanawake, jambo ambalo si kweli.

“Kuna wazalishaji wasio wakweli, wanaandika kwenye vifungashio vya sabuni kuwa sabuni zao zinarudisha bikra kwa wanawake, jambo ambalo
sayansi inakataa na hata wakiulizwa mchanganyiko wa vitu walivyochanganya na vipimo vyake ndani ya sabuni hizo wanashindwa kujieleza,” alisema Alananga.

Meneja huyo alisema, kutokana na mamlaka yake kugundua uwepo wa bidhaa hizo sokoni, mwaka juzi waliandaa mafunzo ya kanuni bora za uzalishaji na ufungashaji kwa wazalishaji 76 mkoani Mbeya lakini mrejesho umekuwa mdogo wa kuhitaji kusajiliwa bidhaa zao katika mamlaka hiyo.

“Wananchi wanaponunua bidhaa yoyote ya kiwandani wawe makini na kuangalia kama bidhaa hiyo ina jina halisi la biashara, tarehe iliyozalishwa bidhaa hiyo, na tarehe ya mwisho ya matumizi, mahali ilipotengenezwa, mhusika aliyetengeneza na mawasiliano ya mtengenezaji,” alifafanua meneja huyo.

Alisema kwa kufanya hivyo ni haki ya mteja na ni matakwa ya kisheria kuhakikisha vitu hivyo vinakuwepo kwenye vifungashio.

Aidha, alisema upotoshaji wa baadhi ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye vifungashio umeleta changamoto kubwa kwa walaji na kwamba TFDA imebaini kuwa katika viwanda vingi vidogo vidogo ndiko kwenye changamoto nyingi kuliko viwanda vikubwa.

“Tunaendelea kufanya ukaguzi madukani na kwenye viwanda vidogo vidogo kwa sababu wengi wanazalisha katika mazingira ambayo sheria hairuhusu kutokana na uchafu uliokithiri ikiwamo vifaa vya kuzalishia, usafi binafsi mfano, ukataji wa kucha, upimaji wa afya, kukohoa na vinginevyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles