‘HAKUNA MADINI YALIYOGUNDULIWA RUANGWA’

0
1184

Mwandishi Wetu, Dodoma


Serikali imesema hakuna uthibitisho wa uwepo wa madini aina ya Coltan yaliyogunduliwa katika wilaya za Ruangwa, Masasi na Newala.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema hayo bungeni leo Jumatano Septemba 5, wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, utaratibu uliotumika katika kuweka alama za mpaka katika wilaya nyingine.

“Madini aina ya Coltan, yamegunduliwa katika wilaya za Masasi, Newala na Ruangwa, lakini serikali imeweka alama za mpaka katika kijiji cha Namndimba Kata ya Chilangala, je serikali haioni kupora rasilimali ya wilaya nyingine kunaweza kusababisha mgogoro, ni lini serikali itamaliza mgogoro huu?” amehoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Nyongo amesema madini yaliyogunduliwa katika wilaya hizo ni ya Graphite ambapo baadhi ya kampuni zimepewa leseni za utafiti na uchimbaji wa madini hayo.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni zake, mmiliki wa leseni anatakiwa kuweka alama zinazoonyesha mipaka ya leseni yake ili jamii inayozunguka maeneo hayo ijue mwisho wa leseni husika.

“Lakini pia alama za Kijiji cha Namdimba, ziliwekwa na Kampuni ya Nachi Resources Limited wakati wa ukusanyaji wa taarifa muhimu, hata hivyo, serikali haina mpango wa kupora rasilimali za wilaya nyingine bali lengo lake ni kuhakikisha rasilimali za madini zinazopatikana katika eneo husika zinawanufaisha wananchi kwa ujumla,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here