HAKIMU KESI YA KINA MBOWE AGOMA KUJITOA

0
219

Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyofurika wafuasi wa Chadema, imezizima kwa ukimya baada ya Hakimu  Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi inayowakabili viongozi tisa wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kugoma kujitoa.

Hakimu Mashauri alitoa uamuzi wa kugoma kujitoa jana mahakamani hapo baada ya kupitia hoja zaidi ya kumi, akiombwa na washtakiwa ajitoe kwa madai hawana imani naye.

“Hoja ya kuomba nijitoe kutokana na masharti ya dhamana niliyotoa, yanayowataka washtakiwa kuripoti polisi kila siku ya Ijumaa, haina mashiko kisheria wala kawaida kwa sababu wangekuwa hawakuridhika nayo wangekata rufaa Mahakama Kuu.

“Ilitolewa sababu kwamba kwa mwonekano wa hakimu hawezi kutenda haki, niko katika benchi hili kwa miaka 22 sasa, sijawahi kuombwa kujitoa kwa sababu za ajabu ajabu kama hizi, sababu hiyo sikuitilia maanani.

“Nimepitia sababu zote za kutaka nijitoe, lakini maombi hayo hayana mashiko ya kutosha kunikataa,” alisema.

Inaendelea………….. Jipatie nakala yako gazeti la MTANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here