24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Gwajima akana kupiga picha za utupu

Elizabeth Joachim , Dar es Salaam

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amekana kuhusika kwenye video ya faragha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuhusisha yeye kuwa imetengenezwa.

Gwajima amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Mei 8, Jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima.

“Hiyo video aliyeisambaza ni mtu mmoja anajiita The Originaleast wa mtandao wa instagram na sijui ameitengeneza hivyo akiwa na maana gani na siku zote ukikuta mtu amerusha tukio la mtu au watu wakiwa chumbani jua nia yake si nzuri.

“Naomba mjiulize ni mwanamume gani anaweza kujirekodi mwenyewe halafu ajiwekee mikono ya baunsa alafu aitume kwenye mitandao lengo la mtu huyu haliwezi kuwa zuri na ana lengo la kunichafua,” amesema Gwajima.

Aidha, Gwajima amesema tayari amesharipoti Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu video hiyo na ameripoti polisi na kupewa RB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles