26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Gumzo Kim Jong-un baada ya kupanda mlima mtakatifu

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

RAIS wa Korea kaskazini, Kim Jong-un amepanda mlima mrefu kuliko yote nchini humo kwa kutumia farasi.

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya hivyo kwani alishawahi kupanda kilele cha urefu wa mita 2,750 huku dhumuni likiwa ni kufanya matangazo muhimu.

Mlima huo ni mahali ambapo baba wa kiongozi huyo wa Korea kaskazini alizaliwa huku pia ni kati ya vivutio vya nchi hiyo.

Kitendo cha kiongozi huyo kupanda mlima wa Paektu kinatajwa kuwa ni kitendo kikubwa cha kihistoria.

Kiongozi huyo ametafakari hatua hiyo ya kupanda mlima Paektu kama kuongoza nchi hiyo huku akisema inahitaji kuwa imara kama mlima huo.

Mara ya mwisho Kim Jong-un kupanda mlima Paektu kumeleta matokeo makubwa na mipango mikubwa iliyofanywa na kiongozi huyo juu ya nchi hiyo.

Inasemekana kuwa kiongozi huyo safari hii, anaweza kubalisha mawazo yake juu ya majaribio ya makombora ya masafa marefu pamoja na silaha za nyuklia.

Huku mazungumzo na utawala wa Marekani yakionekana yametulia  amekuwa akitingwa na shughuli nyingine za kinyumbani na mambo ya kigeni.

Inawezekana Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amepanda mlima huo kama mbinu ya kuelekea kukubaliana na mawazo ya uongozi wa Trump.

Marekani imetakiwa kuja na suluhisho juu ya kusitisha mpango mzima wa nyuklia.

Kim amekuwa akikumbana na vikwazo mbele yake kabla hajatatua mgogoro huo wa nyukliya, lakini anaonekana kama amefeli kuwashawishi Marekani.

Mwanzoni mwa mwezi huu, maofisa wa Korea kaskazini walikutana na maofisa wa Marekani nchini Sweden huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu raisi wa Marekani Trump na Kim walipokutana katika eneo la mpaka wa kati wa Korea mwezi Juni.

Marekani ilidai kuwa ‘maamuzi mazuri na ya busara yalifanyika’. Ikumbukwe kuwa kabla ya mazungumzo hayo Korea Kaskazini ilirusha aina mpya ya kombora ikiwa ni zoezi la 11 kwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles