27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola apigia saluti muziki wa Liverpool

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema vijana wa kocha wa Liverpool, Jurgen Kloop, ndio pekee wamekuwa wakimuumiza kichwa tangu atue Ligi Kuu England.

Manchester City ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu dhidi ya Liverpool ambayo nayo ipo kwenye mbio hizo ikiwa imebakiza michezo miwili.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, kwa sasa analiwinda taji la nane la Ligi Kuu lakini  anaamini Liverpool imekuwa mshindani  mkubwa  tangu awe  kocha  licha ya kukabiliana na ushindani dhidi ya Borussia Dortmund na Real Madrid.

“Katika Ligi Kuu nilizocheza Liverpool imekuwa ikionyesha ushindani mkubwa kwangu tangu kuanza kazi hii ya ukocha. Kila ligi  ukishinda ni jambo zuri lakini pia kuna ugumu wake hata hivyo Liverpool imekuwa  ya kipekee.

“Tumepambana vya kutosha  lakini ni ngumu kupata pointi 100. Lakini  ni jambo gumu kuwa kwenye kiwango kinachofanana kila msimu,” alisema Guardiola wakati akihojiwa na runinga ya Sky Sports.

Guardiola  amepanga kushinda taji la Ligi Kuu England  kwa mara ya pili mfululizo ambapo itakuwa mara ya kwanza  katika historia ya klabu ya Manchester City.

 “Baada ya msimu uliopita kutwaa taji wachezaji wangu nyota bado walikuwa na hamu ya kutwaa tena taji hili.

“Huu ni mchezo wa soka, watu wanaokuja Uwanja wa Etihad msimu huu si kwa ajili ya kukumbuka  soka la kupendeza la msimu uliopita. Huko tulishamaliza.

“Msimu ujao pia hautakuwa sawa kama msimu huu. Kama nikikaa hapa na kukumbuka yaliyopita nitafukuzwa haraka sana.

“Klabu kubwa kama hii kila siku inawaza kubadili makocha kwa kuwa kila msimu inataka kushinda mataji,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles