Na Joseph Lino, Dar es Salaam
Kampuni ya Graphex Mining imetangaza kuwa kuna ongezeko la asilimia 80 ya madini ya grafiti katika mradi wa Chilalo uliyopo Nachingwea nchini Tanzania.
Mradi wa Chilalo sasa utakuwa na tani milioni 16.9 za grafiti zenye kiwango cha graphitic carbon asilimia 10.2 na pamoja na tani milioni 5.2 zlizothibitishwa na tani milioni 11.7 haijathibitishwa kamili (inferred).
Ongezeko hilo linafuatiwa baada kukamilika uchimbaji wa shimo 13 lenye mita 1 365.
Mkurungezi wa Gaphex, Phil Hoskins, alisema kuongezeka kwa hilo shimo katika mradi wa Chilalo inathibitisha kuweko kwaa grafiti bora eneo hilo.
"Kuongezeka kwa rasilimali ya madini inatarajia kuongeza maisha ya mradi huo na kuboresha uchumi, haya ni matokeo bora yatakayosaidia katika mbinu za masoko na maendeleo ya Chilalo ambayo yanatarajiwa kuleta matokeo mazuri kwa wanahisa,” alisema.
Hoskins alisema mradi umetoa thamani ya umuhimu wa uwezo kuendelea na uchimbaji katika mradi wa Chilalo na habari hizi zitakaribisha fedha za uendeshaji wakati mazungumzo yanaendelea.
Mradi wa Chilalo unakadiriwa kuwa na mtaji wa uendeshaji wa dola milioni 74 ambao utaweza kuzalisha tani 69,000 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 10.
Nayo Kampuni ya Volt Resources hivi karibuni ilitangaza kuwa kampuni binafsi ya maabara kutoka German Metallurgical Laboratory ilithibitisha kuwepo kwa grafiti bora katika mradi wa Namangale uliopo mkoani Mtwara.