GOZBERT: NYIMBO ZANGU NI MAISHA HALISI YA WATU WANGU

0
292

Na JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM


MWIMBAJI wa muziki wa Injili nchini, Goodluck, akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Goodluck Gozbert  amesema nyimbo nyingi ambazo amekuwa akiimba, zimetokana na maisha halisi ya watu wake wa karibu na amekuwa akiimba vitu vinavyowagusa watu wake wa karibu ili kutoa funzo kwa watu wa mbali.

“Kuna vitu ambavyo wanadamu wanatakiwa kujifunza kupitia mifano halisi, ndio maana kila wakati ninapoandaa nyimbo basi lazima nitahusisha kisa kilichomtokea mtu wangu wa karibu,” alisema Gozbert.

Alisema mbali na kutumia mikasa iliyowakuta watu wa karibu, pia wakati mwingine vitu anavyoimba vimekuwa vikimhusu yeye binafsi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here