Imechapishwa: Tue, May 8th, 2018

GIGY MONEY: NITAINGIA STUDIO MAPEMA


Na JEREMIA ERNEST    |

VIDEO queens anayefanya vizuri kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amesema hawezi kuvumilia kutoingia studio kwa miezi sita.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Gigy Money, alisema kitendo cha kukaa nje miezi sita kitampotezea mashabiki hivyo hataweza kuvumilia kwa muda wote huo akiwa katika likizo ya uzazi.

“Natamani sana kuingia studio ili mashabiki zangu wasinisahau, ila naambiwa nisubiri hadi mtoto afikishe miezi sita kitu ambacho naona kitanishinda kwa kweli,” alisema.

Alisema alimisi kuvaa baadhi ya mavazi anayoyapenda kwa ajili ya ujauzito aliokuwa nao ikiwamo suruali, vimini na blauzi fupi ‘top’ ambazo hajavaa kipindi chote alichokuwa mjamzito, ila kwa sasa amerudi kwenye mavazi yake kama kawaida.

“Nashukuru nimejifungua salama mtoto wa kike aitwae Mayra, ila nilizikumbuka mno nguo zangu ambazo nilipenda kuzivaa,” alisema.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

GIGY MONEY: NITAINGIA STUDIO MAPEMA