31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

GIGY MONEY ATARAJIA KUITWA MAMA

Na JESSCA NANGAW


MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa ‘Nampa Papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amedai kuwa yupo mbioni kupata mtoto, baada ya mastaa mbalimbali kufanikiwa kupata watoto hivi karibuni.

Msanii huyo anayefanya vyema na kibao chake hicho, amesema amefikia wakati wa kuitwa mama na Mungu akipenda mwakani anatamani hilo litimie.

“Kuitwa mama ni baraka na hakuna mwanamke ambaye hatamani hilo, kikubwa ni mipango tu kwa kuwa huwezi kukurupuka, halafu kingine mtoto ni mipango ya Mungu, unaweza kupanga hivi ikawa vile, sasa naona na mimi ni wakati wangu wa kutimiza hilo,” alisema Gigy.

Alisema pamoja na malezi kuwa na changamoto zake lakini ni jambo ambalo lazima alipitie na amejipanga vyema kutimiza azma yake hiyo aliyojiwekea na mpenzi wake.

Gigy alisema anatarajia kupata mtoto na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye wote kwa pamoja wameridhia jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles