23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

GHANA WAMALIZANA NA KOCHA WAO

ACCRA, GHANA


CHAMA cha soka nchini Ghana (GFA), kimeweka wazi kumalizana na kocha wao msaidizi, Gerard Nus ambaye aligoma kurudi kwao Hispania kwa madai ya kutaka kulipwa fedha zake zote ambazo alikuwa anadai.

Kocha huyo alikuwa anaishi hotelini nchini humo tangu kutangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon, Februari mwaka huu.

Inadaiwa kwamba kocha huyo alikuwa hotelini humo kwa wiki saba, huku akisubiri kulipwa fedha zake kutoka kwa shirikisho hilo la soka nchini Ghana.

Shirikisho hilo limeweka wazi kuwa limefanikiwa kupata fedha za kutosha na kumlipa kocha huyo kila kitu mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari kocha huyo ameondoka kwao nchini Uhispania.

"Nawashukuru watu wote nchini Ghana kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote nilichofanya kazi, ni kumbukumbu nzuri kwangu na taifa hilo ambalo linaonesha watu wake wanapenda sana soka.

“Nilikuwa na furaha kufanya kazi nchini Ghana, lakini muda wangu wa kuondoka umefika na nawatakia kila la heri katika safari ya soka na ninaamini kuna mafanikio makubwa yatatokea nchini humo,” alisema Nus.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirikisho hilo ni kwamba, kulikuwa na mvutano kati ya shirikisho hilo na kocha huyo juu ya gharama za kulipia hotelini ambapo alikuwa anaishi kocha huyo kwa kipindi chote, lakini walifikia makubaliano.

Ghana walikuwa katika kipindi kigumu hasa katika masuala ya fedha mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na kushindwa kuwalipa wafanyakazi wao ikiwa pamoja na kocha mkuu Avram Grant. Wafanyakazi wote waliambiwa warudi nyumbani kwao hadi pale fedha zitakapopatikana, lakini Nus aligoma kuondoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles