Gazeti la Mtanzania limerudi

0
3369

Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya New Habari (2006) Ltd, imesema gazeti la MTANZANIA ambalo lilikuwa limesitishwa kuchapishwa kwa mwezi mmoja, limerudi mitaani kama kawaida kuanzia leo.

Kampuni hiyo, ambayo pia inachapisha magazeti ya Rai, Dimba, Bingwa na The African, ilisitisha uchapishaji wa MTANZANIA wiki moja iliyopita ili kufanya mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya utawala ya kampuni hiyo Dar es Salaam juzi, ilisema gazeti hilo limeanza kutoka leo kama kawaida na kuwahakikishia wasomaji wake kuwa litaendelea kuwapo mtaani. 

“Tunapenda kuutangazia umma na wateja wetu kuwa baada ya kubadili muundo wa uendeshaji na kuwekeza kwenye digital, sasa Mtanzania litaendelea kuwapo kuanzia Jumatatu (leo).

“Hatua ya kurudi mapema kutokana na kukamilika mapema kwa kazi ya kubadili muundo wa uendeshaji wa gazeti tofauti na ilivyotarajiwa awali…tunawashukuru wadau wetu na kuwaomba radhi kutokana na usumbufu uliojitokeza,”ilisema taarifa hiyo.

Mhariri   

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here