GAUNI LA MKWE WA MALKIA KUUZWA MIL 581/-

0
513

BERKSHIRE, UINGEREZA            |              


GAUNI la Meghan Markle, lenye thamani ya pauni 200,000, ambayo ni Sh milioni 581 za Tanzania, linatarajiwa kuwekwa sokoni katika maonyesho ya mavazi ya kifalme mwaka huu nchini Uingereza.

Vazi hilo ambalo lilibuniwa na Clare Waight Keller, litakuwa katika maonyesho ya kifalme yanayotarajiwa kufanyika kwa wakazi wa eneo la Queens, mji wa Berkshire nchini humo.

Gauni hilo linatarajia kuvutia watazamaji wengi, wanaotarajia kuwasili katika maonyesho hayo.

Meghan alifunga ndoa na Prince Harry Mei 19, mwaka huu nchini Uingereza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here