25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Frank Lampard kocha mpya Chelsea

LONDON, ENGLAND

HATIMAYE uongozi wa timu ya Chelsea, jana asubuhi ulimtangaza nyota wao wa zamani Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu wa kutumikia viwanja vya Stamford Bridge.

Lampard amesaini mkataba huo kwa ajili ya kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Maurizio Sarri, ambaye aliondoka na kwenda kujiunga na kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus.

Taarifa za Lampard kwenda kumalizana na Chelsea zilianzia Jumatatu wiki hii baada ya uongozi wa timu ya Derby County kuweka wazi kuwa, kocha huyo hatokuwa na timu kwa siku kadhaa kwa kuwa anakwenda kumalizana na Chelsea.

Lampard alikuwa kocha wa Derby County ambaye anashiriki Ligi daraja la kwanza, alikuwa hapo kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini Derby County walimruhusu staa huyo kwenda kumalizana na timu yake hiyo ya zamani.

Ujio wa Lampard ndani ya Chelsea unaweza kuwapa nafasi nyota wa zamani wa timu hiyo Jody Morris na Chris Jones kuwa miongoni mwa viongozi katika benchi la ufundi.

Lampard mwenye umri wa miaka 41, ambaye alitajwa kuwa kiungo bora katika kikosi cha Chelsea wakati wake, aliweza kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja, Kombe la Europa mara moja, Kombe la FA mara nne na Kombe la Ligi mara mbili.

Kipindi cha miaka 13 aliyokaa Chelsea akiwa mchezaji, alicheza jumla ya michezo 640, huku akifanikiwa kufunga mabao 209 na kupiga pasi za mwisho 150.

Kocha huyo amejiunga wakati ambao Chelsea imefungiwa kufanya usajili kutokana na kutumikia kifungo baada ya kufanya makosa ya kusajili wachezaji wenye umri chini ya miaka 18, hivyo Chelsea msimu ujao mbali na kutumia wachezaji wakongwe, lakini watatumia baadhi ya wachezaji kutoka timu za vijana kwa ajili ya kuwapa uzoefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles