27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Filamu kupinga mauaji ya albino kuandaliwa

albinoNA JOHN MADUHU, MWANZA
WAIGIZAJI wa filamu nchini, wanatarajia kuungana katika filamu moja itakayokuwa ikipinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’, alizungumza na MTANZANIA hivi karibuni, wakati wa kongamano la amani lililoandaliwa na maaskofu na masheikh wa Mkoa wa Mwanza.
JB ambaye alikuwa ameongozana na wasanii wengine kama Mzee Majuto na Mrisho Mpoto, alisema mchakato wa kuandaa filamu hiyo umeanza.
“Tumeguswa na mauaji ya walemavu wa ngozi, ambayo yamekuwa yakitokea kila mara kanda ya ziwa, tutatengeneza filamu ambayo kila mtu akipata nafasi ya kuitazama itafikisha ujumbe wa kuacha kufanya mauaji,” alisema JB.
Kwa upande wake, Mzee Majuto, alisema umefika wakati suala la mauaji ya watu wenye ulemavu yakamalizika na kukomeshwa kabisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles