23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

FATMA KARUME: NINA BARAKA ZA LISSU URAIS TLS

Na ELIZABETH HOMBO – DAR ES SALAAM


WAKILI wa kujitegemea, Fatma Karume, amesema ana baraka za Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, kugombea urais katika chama hicho baada ya muda wa mwanasheria huyo machachari kwisha.

Uchaguzi wa TLS unatarajia kufanyika Aprili 14, ambapo Lissu aliye kwenye matibabu nchini Ubelgiji, hatagombea tena baada ya kumaliza mwaka mmoja wa uongozi wake.

Kutokana na kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, mwaka jana na kukaa kwenye matibabu nje ya nchi kwa muda mrefu, Lissu anakuwa ametumikia nafasi yake kama Rais wa TLS kwa miezi sita pekee.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Fatma ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alisema mwanzoni hakuwa tayari kugombea urais wa TLS lakini baadaye akashawishiwa na mawakili vijana akakubali.

“Yalikuwa maamuzi magumu sana kwa sababu sikutaka, nilikuwa naombwa na vijana kwamba Fatma chukuwa fomu ugombee tutakuchagua nikasema hapana nina majukumu mengi.

“Nakumbuka ilipofika Alhamisi kuna kijana mmoja akanifuata akaniambia nakuomba uchukue fomu nikamwambia siko interested kwa sababu nilikuwa nataka nijipunguzie majukumu.

“Sasa baadaye nilivyojiuliza kujipunguzia huku majukumu ina maana nafikiria watu au mimi mwenyewe nikasema huu utakuwa ubinafsi…baada ya kutafakari nikamtumia message yule kijana kwamba achukue fomu ajaze na sehemu ya wadhamini halafu aniletee nisaini.

“Ujue nilikuwa siamini kama atafanya hivyo, lakini ilipofika Ijumaa namwona yule kijana anafika ofisini kwangu na fomu pamoja na sehemu ya wadhamini isipokuwa sehemu yangu, hivyo nikajaza na kusaini sasa mtu kama huyo utamwangusha kweli,” alihoji Fatma.

Mwanasheria huyo alisema baada ya kujaza fomu akampigia simu Lissu na kumweleza kuhusu hilo na akapata baraka zote.

“Nadhani kila mtu anajua kuwa Lissu ni rafiki yangu na ninampenda sana na nikizungumza naye napata faraja, napata furaha, huwa tunataniana sana. Hivyo baada ya kujaza fomu nikampigia kumshirikisha na akanipa baraka zote.

“Ilikuwa lazima nizungumze na Lissu kwa sababu yaliyotokea mnayajua, urais wake ulikatishwa katikati na hajaweza kutimiza yale aliyoahidi kuyatimiza, hivyo kitu kama hicho kimemtokea mwenzako na unagombea lazima uzungumze na mwenzako upate baraka,” alisema wakili huyo.

 

Inaendelea…………………. kwa maelezo zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles