27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

FAO UPOTEVU WA AJIRA LAJA

NA RAMADHAN HASSAN

BUNGE limeelezwa kwa kutambua changamoto ya kipato inayowakabili wafanyakazi pale wanapopoteza ajira, Serikali itawasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii yatakayoanzia fao la upotevu wa ajira.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni (CCM).

Chegeni alidai kuwa, mafao ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mashirika mengi ya hifadhi ya jamii yamekuwa na utata kuhusiana na fao la kujitoa.

“Je, Serikali inatoa tamko gani, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuunganisha mifuko hiyo na kuondoa mkanganyiko kwa wanachama?” alihoji Chegeni.

Akijibu swali hilo, Mavunde alisema kwa kutambua changamoto ya kipato inayowakabili wafanyakazi pale wanapopoteza ajira, Serikali itawasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria za hifadhi za jamii yatakayoanzia na upotevu wa ajira.

Mavunde alisema kwa mujibu wa mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Namba 102 wa mwaka 1952, fao la kujitoa si miongoni mwa mafao yaliyoainishwa katika mkataba huo.

Alisema kwa Tanzania, fao la kujitoa ni utaratibu wa wanachama kujitoa na kuchukua mafao yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii inayotoa mafao ya pensheni kabla ya kufikisha umri wa kustaafu.

“Serikali inatambua changamoto ya wingi wa mifuko inayokabili  sekta ya hifadhi ya jamii, ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali ilifanya tathmini ya mifuko ya mifuko yote  ya pensheni kwa lengo la kuangalia uwezekano wa namna bora ya kuiunganisha,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles