24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

FALSAFA  YA KUTOA MIKOPO KWA UTARATIBU WA MURABAH

Na Jamal Issa Juma


UJIO wa benki zinazotoa huduma za kibenki katika utaratibu unaokubalika katika Uislamu umeleta huduma mbadala za kibenki kwa watu wote na kusaidia kukuza wigo wa wateja hasa wale ambao walikuwa wanaacha kutumia huduma za kibenki kwa sababu ya uwepo wa riba.

Utaratibu wa mikopo katika benki zenye kufuata utaratibu unaokubaliwa na Uislamu kwa kiwango kikubwa umefungamana na huduma au bidhaa mbalimbali. Ni mpangilio mzuri kwa yeyote anayetaka kuutumia kwani unafaida kwa pande zote husika.

Benki za kiislamu zina namna nyingi ya kuwawezesha au kutoa mikopo kwa wateja wake, njia mojawapo nikuwauzia wateja wake huduma au bidhaa mbalimbali wanazohitaji kwa faida.

Utaratibu huu hujulikana kama Murabah.

Utaratibu huu una manufaa makubwa kwa benki, mteja na kwenye uchumi kwa ujumla. Kama nchi tungefaa tuupigie debe kwani unawezesha kufanya makubwa bila hasara yoyote.

Kwa upande wa benki husaidia kukabiliana na udanganyifu wa wateja ambao wanaomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara au mradi fulani kisha wanapopata mkopo huzielekeza fedha hizo kwenye shughuli nyingine tofauti kabisa.

Hali hii hua na athari kubwa kwa  benki hasa pale ambapo mteja ameelekeza mkopo sehemu isiyo na tija au mapato sawa na biashara au mradi ambao umefanyiwa upembuzi na benki wakati alipoomba mkopo kwani mara nyingi katika hali hii wateja hushindwa kulipa vizuri mikopo yao kwa wakati. Hivyo basi benki huchafua vitabu vyake kwa kuwa na mikopo mingi isiyofanya vizuri.

Kwa kutumia utaratibu wa Murabah jambo hili huweza kuepukika kwani mteja hapewi fedha bali benki hununua na kumuuzia bidhaa au huduma anayoihitaji na malipo wakati wakununua bidhaa hizo hulipwa moja kwa moja kwa msambazaji/muuzaji.

Kwa upande wa mteja humsaidia kuelekeza mkopo kwenye shughuli iliyokuwa na tija hivyo kumudu kufanya marejesho jambo ambalo hupunguza hatari ya mteja kuuziwa rehani aliyoweka benki ilikupata mkopo. Patamu hapo!

Pia mteja atakuwa amepata mkopo wa bidhaa ambazo atazitumia kutimiza malengo yake kama vile kukuza mtaji wake, kujenga na kadhalika.

Aidha, katika utaratibu huu unamanufaa makubwa katika uchumi kwani huunganisha moja kwa mojabenki au mfumo wakifedha na shughuli halisi za uzalishaji.

Kwani uchumi umejengwa katika nguzo kubwa ya uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa na huduma mbalimbali. Utaratibu huu wamurabaha umejikita katika kubadilishana bidhaa kwa fedha hivyo huifanya benki kushiriki moja kwamoja katika shughuli za kibiashara na uchumi.

Utaratibu huu ni muhimu sana katika kuzishirikisha benki katika uchumi wa viwanda kwani benki huweza kutoa mikopo ya moja kwa moja katika kuanzisha na kuendeleza viwanda kwa kununua na kuwauzia wawekezaji mashine, ardhi na nyenzo nyingine zinazohitajika.

Pia uchumi wa viwanda hutegemea pia shughuli za biashara na usambazaji wa bidhaa hizo kwa walaji ambapo benki inaweza kutumia utaratibu huu kununua bidhaa kutoka viwandani au kwa wasambazaji na kuwauzia wafanyabiashara kwa mkopo ili kuwawezesha kufanyabiashara hiyo.

Kwa ufupi utaratibu  huu ni wauhakika katika kuunganisha benki na shughuli za uchumi na hautoi mwanya wa kuelekeza fedha katika shughuli zisizonatija katika uchumi.

Taasisi zakifedha kama benki zinaweza kutumia murabaha kama njia ya kuwawezesha wateja wao kununua bidhaa mbalimbali na pale wanapokuwa wanahitaji bidhaa fulani lakini hawana uwezo wa kifedha wakununua kwa kufanya malipo papohapo.

Benki inaweza kununua bidhaa fulani na kumuuzia mteja wake kwa faida kwa njia ya mkopo. Mteja atalipa mkopo huo kwa awamu na kwa muda ambao watakubaliana na benki.

Murabaha sio mkopo unaotolewa kwariba, bali ni uuzaji wa bidhaa kwamkopo kwafaida inayowekwa juu ya gharama.

Faida hupatikana kwa kununua na kuuza bidhaa kwaziada wakati riba hupatikana kwakutoafedha kwamteja kwamakubaliano yakurejesha naziada. Faida hupatikana kwakubadilisha bidhaa kwafedha na riba hupatikana kwa kubadilishana fedha kwafedha za ainamoja. Utaratibu wa kubadilishana fedha kwa fedha hauna tija ya moja kwamoja kwenye uchumi ukilinganisha na utaratibu wakubadilishana fedha kwa bidhaa au huduma.

Katika makala nyingine inayofuata, Mwenyezi Mungu akitujalia, tutaeleza hasa namna gani utaratibu huu unatekelezwa na benki zinazofuata utaratibu huu wa Murabah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles