24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

EVRA AONYESHWA KADI NYEKUNDU KABLA YA MCHEZO

MARSEILLE, UFARANSA

BEKI wa pembeni wa klabu ya Olympique Marseille, Patrice Evra, juzi alioneshwa kadi nyekundu kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kombe la Ligi ya Europa dhidi ya Vitoria Guamares.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United na klabu ya Juventus, alioneshwa kadi hiyo baada ya kumpiga teke shabiki wake wakati wakipasha misuli kuelekea mchezo huo.

Baadhi ya mashabiki wa Olympique Marseille walionekana kuwazonga wachezaji wao mara kwa mara na kuwazomea jambo ambalo mchezaji huyo alionekana kuchukizwa na kuamua kuwafuata ili kuzungumza nao, lakini maelewano bado hayakuwa mazuri, hivyo aliamua kumrukia shabiki huyo na kumpiga shingoni.

Tukio hilo lilimfanya Evra aonyeshwe kadi nyekundu moja kwa moja na kuukosa mchezo huo japokuwa bado ulikuwa haujaanza. Hata hivyo, katika mchezo huo, Evra hakuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wangeanza kwenye kikosi cha kwanza, lakini alikuwa kwenye kikosi cha akiba. Katika mchezo huo, Olympique Marseille walikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Vitoria Guamares.

Kutokana na kitendo alichokifanya Evra, Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA), kimeweka wazi kuwa kinatarajia kuchunguza zaidi tukio hilo na kutoa adhabu kubwa zaidi ya hiyo ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa.

Kocha wa klabu hiyo ya Marseille, Rudi Garcia, ameonekana akimtetea Evra kwa kusema kwamba, mashabiki walimwandama sana na ndio maana aliamua kuchukua hatua hiyo kwa hasira.

“Nadhani mashabiki walikuwa wakali sana hata sijui kwanini, kitendo hicho kilimfanya Evra achukie na kufikia hatua ya kumpiga shabiki wake, hakukusudia kwenda kumpiga lakini kutokana na maneno yao hicho kitu kikatokea,” alisema Garcia.

Tukio ambalo amelifanya Evra kumpiga shabiki linafananishwa na nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa, Eric Cantona mwaka 1995. Kitendo hicho kilimfanya afungiwe kujihusisha na soka kwa miezi 9.

Hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Evra kukumbana na kifungo cha muda mrefu na Chama cha Soka barani Ulaya endapo kitafanya uchunguzi na kuthibitisha kuwa mchezaji huyo alifanya kosa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles