Imechapishwa: Fri, Apr 20th, 2018

EU WATISHIA KUIWEKEA VIKWAZO VENEZUELA

BEIJING, CHINA


UMOJA wa Ulaya (EU) umeonya utaiwekea vikwazo zaidi Venezuela na kutishia kuchukua hatua zaidi kama hizo iwapo demokrasia haitazingatiwa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.

Mkuu wa Sera za Nje wa EU, Federeca Moghereni, alisema katika taarifa yake kuwa amesikitishwa na uamuzi wa maofisa wa Venezuela chini ya Rais Nicolas Maduro.

Alisema haikuwa busara kwa maofisa hao kuamua kuitisha uchaguzi wa rais na Bunge Mei 20 bila kupatikana mwafaka juu ya taratibu zinazokubalika kuhusu mchakato huo.

Aliongeza kuwa Umoja wa Ulaya utafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi na kuwa uko tayari kuchukua hatua dhidi ya uamuzi au vitendo vyovyote vinavyolenga kuikandamiza demokrasia na utawala wa sheria nchini Venezuela.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

EU WATISHIA KUIWEKEA VIKWAZO VENEZUELA