26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

EU, URUSI, UKRAINE KUTETA KUHUSU MKATABA WA  GESI

BRUSSELS, Ubelgiji


RAIS  wa Kamisheni ya Nishati  wa Jumuiya ya nchi za Ulaya,EU,   Maros Sefcovic, amesema kwamba tayari ameshafanya mazungumzo  ya awali na nchi za Urusi na  Ukraine ya kuongeza mkataba wa gesi kuendelea kupitia  Ukraine pindi mkataba wa sasa utakapomalizika ifikapo mwakani.

Sefcovic alitoa kauli hiyo juzi katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters na akasema kuwa mazungumzo ya kina yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

“Tumeshafikia makubaliano ya wali na washirika wetu  hao wawili, Ukraine na Urusi na tumewaarika kufanya mazungumzo ya kina,”alisema Rais huyo wa Kamisheni ya Nishati Ulaya.

“Mazungumzo ya kina yatafanyika hivi karibuni na jambo na muhimu litakuwa ni kuhusu kuendelea kuagiza gesi na tunataka iendelee kupitia Ukraine mara baada ya mkataba huu kumalizika mwakani,”aliongeza, Sefcovic

Alisema kuwa Rais wa Urusi,  Vladimir Putin naye alishamuhakikishia kuwa Serikali ya Moscow, tayari imeshafanya mazungumzo na  Ukraine ili gesi hiyo iendelee kupitia nchini humo, baada ya wiki iliyopita kukutana na Kansela wa Ujerumani,  Angela Merkel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles