24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Eto’o avuliwa majukumu ya ukocha

Samuel-Eto’oANKARA, UTURUKI

NAHODHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o, amepokonywa majukumu yake kama kaimu kocha mchezaji katika klabu ya Antalyaspor ya nchini Uturuki.

Nafasi yake imechukuliwa na Jose Morais, ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Chelsea, chini ya Mreno mwenzake, Jose Mourinho hadi Desemba mwaka jana.

Morais, ambaye alihusishwa na kuhamia Swansea City, pia alikuwa na Mourinho wakati anaitumikia klabu ya Real Madrid na Inter Milan.

Eto’o alipewa majukumu ya kuifundisha klabu hiyo mapema Desemba mwaka jana baada ya kuchukua nafasi ya Yusuf Simsek ambaye alifukuzwa kazi, hivyo Eto’o alifanikiwa kushinda michezo yake miwili ya kwanza kabla ya kushindwa michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na Chelsea, alikuwa na mkataba na klabu hiyo ya nchini Uturuki wa miaka mitatu kama mchezaji, hivyo baada ya kuvuliwa majukumu ya ukocha ataendelea kuwa mchezaji wa kawaida kama ilivyo awali katika mkataba wake.

Morais mwenye umri wa miaka 50, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwenye sherehe ya klabu hiyo ambayo iliongozwa na mwenyekiti wa Antalyaspor, Gultekin Gencer.

Hata hivyo, kocha huyo ameahidi makubwa msimu huu katika klabu hiyo ikiwa ni miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles