24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ethiopia yaiumbua Ikulu ya Kenya

Tolossa Shagi
Tolosa Shagi

ADDIS ABABA, ETHIOPIA

SERIKALI ya Ethiopia imekana taarifa za Ikulu ya Nairobi kwamba imesaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.

Badala yake Serikali imesema makubaliano yaliyosainiwa na Kenya yalilenga kufanya tathimini juu ya uwezekano na manufaa ya mradi huo, limeripoti gazeti la Ethiopia.

Waziri wa Madini, Petroli na Gesi Asilia, Tolossa Shagi, alikana kutia saini makubaliano rasmi ya kujenga bomba hilo, na hivyo kutofautiana na tamko lililotolewa na Ikulu ya Nairobi.

“Hatujasaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta. Hiki mlichosikia ni ripoti yenye makosa,” Shagi aliwaambia wanahabari.

Alisema: “Tumekubaliana kuchukua muda zaidi kutathimini suala hilo. Tutafanya mazungumzo zaidi na tunaweza kusaini mkataba iwapo tutaona mradi huu una manufaa ya kiuchumi na kiufundi. Lakini naweza kuthibitisha kwenu hatukusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.”

Kwa mujibu wa waziri, Kenya iliwasilisha wazo la ujenzi wa bomba la mafuta kwa Serikali yake, na Addis Ababa ilikubali kutathimini ufanisi wake kwanza.

Hilo linapingana na tamko lililotolewa mwezi uliopita na Ikulu ya Nairobi, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn alipotembelea Nairobi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles