27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

ELIMU YA UKIMWI YATOLEWA KWA MAKUNDI MAALUM

Na SAMWEL MWANGA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Maswa   imeanza kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi kwa vijana   katika makundi maalum katika maeneo ya kazi.

Hayo yamefanyika baada ya baadhi ya wahudumu wa kike katika baa na nyumba za wageni wilayani humo kuiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kuwapatia elimu ya Ukimwi   wawe katika mazingira mazuri ya kujiepusha na maambukizi.

Wahudumu hao walikuwa wakizungumza na waandishi wa habari   baada ya kumalizika   semina ya kudhibiti Ukimwi kwa viongozi iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Walisema  ugonjwa huo bado ni tishio kwa kuwa hauna dawa wala kinga wakati  watu wanaendelea kuambukizana virusi vinavyosababisha Ukimwi.

“Ugonjwa wa Ukimwi bado ni tishio katika maisha yetu sisi binadamu kwa sababu  hadi sasa hauna dawa wala kinga na bado watu wanaendelea kuambukizana virusi vinavyosababisha ugonjwa huu na athari zake zinaonekana wazi katika jamii,”alisema Jesca John.

Alisema   wao wana ufahamu mdogo juu ya ugonjwa huo na hawapendi kuzungumzia kwa uwazi jinsi unavyoathiri .

Jesca alisema na ndiyo sababu  wengi wao wamekuwa wakiambukizwa kwa kukosa elimu ya Ukimwi lakini kwa sasa wamepata uelewa mzuri juu ya maambukizi mapya.

Mwajuma Ally, mhudumu wa baa alisema   ana zaidi ya miaka 10 katika kazi hiyo lakini hajawahi kupatiwa elimu juu ya ugonjwa huo licha ya serikali na asasi nyingine kufahamu mazingira ya kazi zao jinsi yanavyochochea maambukizi ya ugonjwa huo.

 Naye Zamuda Hassan alisema   amekuwa akisikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba watumishi wa serikali, asasi binafsi, mashirika ya umma na watu wengine wakishiriki semina juu ya ugonjwa huo.

Alisema  hata siku moja hawajawahi kusikia wahudumu wa baa wameshirikishwa katika semina hizo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Ndila Mayeka alisema halmashauri hiyo imeamua kutoa elimu hiyo baada ya kubaini kuwa hali iliyopo kwenye baa nyingi inatisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles