24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ed sheeran atajwa kuwa msanii tajiri zaidi duniani

Mwanamuziki wa nchini Uingereza, Ed sheeran ametajwa kuwa ndiye msanii tajiri zaidi katika kundi la watu maarufu wenye umri wa chini ya miaka 30.


Utajiri wa Ed sheeran umeongezeka karibu mara mbili ndani ya miezi 12 ambapo inakadiriwa kuwa paundi milioni 170 na hivyo kumfanya afanikiwe kumnyang’anya nafasi ya kwanza mwanamuziki Adele.

Nafasi ya pili imechukuliwa na muigizaji wa filamu Daniel Radcliffe ‘Harry Potter’ ambaye thamani yake ni paundi milioni 90.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanamuziki Harry Styles ambaye alikuwa katika kundi maarufu la muziki nchini humo la One Direction ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 64.

Mwaka jana Adele alishika nafasi ya kwanza akiwa na thamani ya paundi milioni 147.5 lakini yeye alitimiza miaka 31 Mei 5 mwaka huu na hivyo hakupata nafasi ya kushirikishwa katika awamu hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles