27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ebola yaingia Uganda, WHO yaonya kusambaa

ENTEBE-UGANDA

MTOTO wa kiume wa miaka mitano ambaye anakuwa wa kwanza kuthibitika kuwa na ugonjwa wa Ebola nje ya mipaka ya Kongo  amefariki dunia nchini Uganda.

Mamlaka za nchini Uganda zimesema kuwa mtoto huyo ambaye alifariki Juzi usiku, mdogo wake wa miaka mitatu na bibi yake mwenye umri wa miaka 50 nao pia wanatibiwa ugonjwa huo.

Wagonjwa hao wametengwa hospitalini karibu na mpaka wa Kongo.

Shrika la Afya Duniani (WHO) imeiweka tayari Kamati maalumu kwa ajili ya kushauri iwapo hali ya hatari itangazwe, baada ya maofisa kuthibitisha kama mlipuko wa ugonjwa wa Ebola sasa  umevuka mipaka ya Kongo.

Wizara ya Afya ya Kongo imeeleza kuwa mtoto huyo aliyefariki nchini Uganda yeye na familia yake ya watu watano walitokea nchini Kongo Jumatatu jioni wiki hii.

Mtoto huyo anaweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kufa kwa ugonjwa wa Ebola nje ya Kongo tangu mlipuko huo uanze mwezi Agosti mwaka huu.

Waziri wa afya Uganda Jane Ruth Aceng amewaambia wanaandishi habari kwamba familia ya mtoto huyo wanaangaliwa, wakiwemo wawili walionyesha kuwa na dalili za kama za ugonjwa wa Ebola.

Tayari wahudumu 4, 700 nchini Uganda wamepewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Mlipuko huo wa sasa ambao umegharimu maisha ya watu 1,400 unaweka historia ya pili kwa kusababisha vifo vingi Kongo.

Tayari WHO  imeonya kuwa ugonjwa huo  unaweza kusambaa katika maeneo mengine ya ukanda huo. 

Nchini Kongo, mlipuko wa ugonjwa huo umeathiri majimbo ya Kaskazini-mashariki, ambako kuna mipaka ya Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

Kati ya mwaka – 2013 na 2016  Ebola ilikuwa janga Afrika ya Kati ambako ilishuhudia a vifo vya watu 11, 310.

Ebola ni ugonjwa unao sambaa haraka na husababisha vifo vya asilimia 50 ya waathirika

Dalili za awali ni homa ya ghafla, uchovu kupita kiasi, maumivu ya mishipa na koo.

Dalili za hatari ni kutapika, kuharisha, kutoka damu ndani na nje ya mwili.

Ebola huwapata binadamu wanapogusana na wanyama walioathirika wakiwemo sokwe mtu, popo na paa.

Watu wanaambukizwa endapo damu zao na zimebeba vijidudu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles